Maandamano makubwa ya kupinga sera zilizofeli za Benjamin Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i140368-maandamano_makubwa_ya_kupinga_sera_zilizofeli_za_benjamin_netanyahu
Wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel wamefanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali wakipinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo wamezitaja kuwa zimeshindwa.
(last modified 2026-08-03T02:43:36+00:00 )
Aug 03, 2026 02:40 UTC
  • Maandamano makubwa ya kupinga sera zilizofeli za Benjamin Netanyahu

Wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel wamefanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali wakipinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo wamezitaja kuwa zimeshindwa.

Maeneo mbalimbali yanayokaliwa kwa mabavu na ambayo yamepewa jina bandia la Israel, ikiwemo makutano ya Karkur kati ya miji ya Tel Aviv na Haifa pamoja na maeneo mengine, yameshuhudia maandamano makubwa ya mamia ya maelfu ya watu kupinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo waandamanaji wanazitaja kuwa zimeshindwa ma kugonga mwamba.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Quds (Qudsna), maandamano hayo yamefanyika huku maelfu ya watu wakikusanyika pia mbele ya makao makuu ya Wizara ya Vita ya Israel mjini Tel Aviv, wakilaani hatua na vitendo vya walowezi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa taarifa za Kanali ya 12 ya televisheni ya Israel na gazeti la Haaretz, miongoni mwa walioshiriki maandamano hayo alikuwa Ofer Cassif, mbunge wa Muungano wa Hadash katika Knesset (Bunge la Israel).

Wakati huohuo, mamia ya maafisa wa zamani wa usalama wa Israel hivi karibuni walimtaka Rais wa Marekani, Donald Trump, kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na walowezi katika Ukingo wa Magharibi. Maafisa hao walionya kuhusu madhara ya vitendo hivyo kwa usalama wa Israel na maslahi ya Marekani.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, kwa wiki kadhaa sasa, Ukingo wa Magharibi umeshuhudia kuongezeka mashambulizi yanayofanywa na jeshi la Israel pamoja na walowezi dhidi ya Wapalestina.