-
Netanyahu aiomba US iishinikize Misri ipunguze kujiimarisha kijeshi kwenye Peninsula ya Sinai
Sep 21, 2025 09:10Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameiomba serikali ya Marekani iishinikize Misri ipunguze hatua za kujizatiti kijeshi katika eneo la Peninsula ya Sinai. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana Jumamosi na tovuti ya habari ya nchini Marekani ya Axios.
-
Mayahudi wa Othodoksi waanza kuandamana New York dhidi ya Netanyahu kabla hajaelekea UN
Sep 18, 2025 10:13Mamia ya Wayahudi wa madhehebu ya Othodoksi wamefanya maandamano katika jiji la New York kupinga ushiriki wa waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa itakayofanyika wiki ijayo.
-
Kwa mara ya kwanza Netanyahu akiri kwamba Israel imenasa kwenye kinamasi cha 'kutengwa' kimataifa
Sep 16, 2025 06:47Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekiri kwa mara ya kwanza hadharani kwamba utawala huo ghasibu unatumbukia kwenye lindi la "kutengwa," wakati mashinikizo ya kimataifa yakiwa yanaongezeka dhidi ya vita vinavyoendelezwa na jeshi la kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na dhidi ya sera za serikali ya Netanyahu ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali ya chuki na ubaguzi.
-
HAMAS: Kufanya ibada ya Kiyahudi Rubio na Netanyahu kwenye Ukuta wa Buraq ni kuitusi Quds na Msikiti wa Al Aqsa
Sep 15, 2025 06:25Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, hatua ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, pamoja na Benjamin Netanyahu, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC ya kufanya ibada ya Kiyahudi kwenye Ukuta wa Buraq, ambayo ni sehemu isiyotenganika na Msikiti wa Al-Aqsa, ni kuuvunjia heshima waziwazi utakatifu wa msikiti huo na ni ukiukaji wa hadhi ya kihistoria na kisheria ya Baitul Muqaddas.
-
Netanyahu aapa hakutakuwa na Dola la Palestina, asisitiza ardhi yote ni milki ya wazayuni
Sep 12, 2025 10:28Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuwa, hakutakuwa na dola la Palestina, na kusisitiza kwamba ardhi zote za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu ni milki ya wazayuni.
-
Netanyahu na jeshi la kizayuni watoa vitisho vikali kwa Wapalestina: Ondokeni Ghaza sasa hivi!
Sep 09, 2025 10:28Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ametishia kile anachokiita operesheni kali ya ardhini katika mji wa Ghaza, huku akitoa vitisho kwa Wapalestina walioko katika mji huo kwa kuwataka waondoke sasa hivi.
-
Kwa nini maandamano yameshadidisha hali mbaya ya mgogoro Israel?
Aug 19, 2025 10:26Mgogoro wa hivi sasa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kushadidi maandamano yanaashiria kudhoofika muundo wa kisiasa na kiusalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Borrell amkemea Netanyahu kwa kutaka Trump apewe Tuzo ya Amani ya Nobel
Jul 10, 2025 06:09Mkuu wa zamani wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amekemea pendekezo la waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu la kutaka rais wa Marekani Donald Trump atunukiwe Tuzo ya Amani ya Nobel, akilielezea hilo kuwa ni hatua iliyochukuliwa na "mtu anayeaminika kuwa mhalifu wa kivita" kwa ajili ya "muuzaji wake mkuu wa silaha".
-
Seneta, mbunge wa US walaani mhalifu wa vita Netanyahu kukaribishwa tena White House
Jul 09, 2025 08:13Seneta wa Marekani Bernie Sanders na Mbunge Ilhan Omar wamelaani waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kukaribishwa tena mjini Washington na katika Ikulu ya White House wakati utawala huo ghasibu unaendeleza vita vya kinyama na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 57,500 wameuawa shahidi hadi sasa.
-
Ni marufuku wenye paspoti za Israel kuingia Maldives kutokana na jinai za Wazayuni Ghaza
Apr 16, 2025 02:20Maldives haitawaruhusu tena watu wenye pasi za kusafiria za utawala wa Kizayuni wa Israel kuingia nchini humo.