-
Marufuku ya kuingia wanariadha wa utawala wa Kizayuni nchini Indonesia
Oct 27, 2025 04:30Indonesia inachukulia marufuku ya kuingia wanariadha wa utawala Kizayuni wa Israel katika nchi hiyo kuwa haki yake halali.
-
Ni mambo gani yameifanya Israel itengwe kisiasa na kijamii kiasi hiki?
Oct 24, 2025 02:32Israel inakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa katika historia yake. Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa utawala wa Kizayuni, alikiri hivi karibuni katika kikao cha kamati moja ya Knesset kwamba Israel hivi sasa iko katika mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa katika historia yake.
-
Unafiki wa Ulaya mkabala wa Gaza: Biashara na Israel au kuheshimu haki za binadamu?
Oct 23, 2025 02:29Umoja wa Ulaya utarejesha uhusiano wake wa kibiashara wa upendeleo na Israel hatua kwa hatua kwa kisingizio cha kutekelezwa usitishaji unaolegalega wa mapigano huko Gaza.
-
Hamas: Israel lazima igharamie ujenzi mpya wa Gaza
Oct 21, 2025 11:31Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, Mousa Abu Marzouk ametoa wito kwa Israel kufadhili kikamilifu ukarabati na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza, akitaja uharibifu mkubwa na haki za Wapalestina zaidi ya milioni mbili ambao wamepoteza makazi yao, makazi na riziki.
-
Amir wa Qatar: Vita vya Israel dhidi ya Ghaza si kingine chochote ila ni mauaji ya kimbari
Oct 21, 2025 07:00Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amesema, vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza si kitu kingine ila ni mauaji ya kimbari sambamba na kuulaani utawala huo ghasibu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Netanyahu ajigamba kuwa siku ya Jumapili Israel iliidondoshea Ghaza tani 153 za mabomu
Oct 21, 2025 07:00Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amejigamba kuwa jeshi lake lilishambulia Ukanda wa Ghaza siku ya Jumapili kwa tani 153 za mabomu, ambayo ni sawa na kukiri kwamba utawala huo ghasibu umekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano uliyofikia na harakati ya Hamas kupitia mpango uliopendekezwa na Rais wa Marekani.
-
Mwakilishi wa US adai vita vya Israel dhidi ya Lebanon haviepukiki ikiwa Hizbullah haitapokonywa silaha
Oct 20, 2025 09:40Tom Barrack, balozi wa Marekani nchini Uturuki na mjumbe maalumu wa masuala ya Syria, ametoa onyo la kutisha kwa Lebanon akiitaka ama iipokonye silaha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchi hiyo Hizbulla au ikabiliwe na mashambulizi mengine ya Israel na migogoro ya kiuchumi na kisiasa.
-
Ripoti: Asilimia 97 ya shule za Gaza zimeharibiwa kwa mashambulizi ya Israel
Oct 20, 2025 03:28Ripoti rasmi zinasema, mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel yameharibu asilimia 97 ya shule za Ukanda wa Gaza na hivyo kuhatarisha mustakbali wa kielimu wa wanafunzi laki tatu wa Kipalestina katika eneo hilo.
-
Iran yailaani Israel kwa kuendelea kuua wanawake na watoto Gaza
Oct 19, 2025 06:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baghaei amelaani ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel, likiwemo shambulio la hivi karibuni dhidi ya gari lililokuwa limebeba familia ya Kipalestina wakati ikirejea kwenye makazi yao.
-
ICC yatupilia mbali rufaa ya Israel dhidi ya hati za kutiwa nguvuni Netanyahu na Gallant
Oct 19, 2025 02:41Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imekataa ombi la utawala wa kizayuni wa Israel la kukata rufaa dhidi ya hati za kukamatwa waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita wa utawala huo ghasibu Yoav Gallant kuhusiana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi la kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.