Hizbullah yawataka walowezi wa Kizayuni kuondoka karibu na mpaka wa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137192-hizbullah_yawataka_walowezi_wa_kizayuni_kuondoka_karibu_na_mpaka_wa_lebanon
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imewataka walowezi wa vitongoji haramu katika mpaka wa pamoja wa Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel kuondoka katika eneo hilo mara moja.
(last modified 2026-03-06T04:40:00+00:00 )
Mar 06, 2026 04:40 UTC
  • Hizbullah yawataka walowezi wa Kizayuni kuondoka karibu na mpaka wa Lebanon

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imewataka walowezi wa vitongoji haramu katika mpaka wa pamoja wa Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel kuondoka katika eneo hilo mara moja.

Taarifa iliyotolewa mapema leo Ijumaa na Hizbullah imeeleza kuwa: Onyo kwa wakazi wote wa vitongoji haramu vya eneo la kaskazini; Mnatakiwa kuondoka katika vitongoji vyote vilivyoko umbali wa kilomita 5 kutoka kwenye mstari wa mpaka. 

Hizbullah awataka walowezi hao kuondoka na kuelekea upande wa kusini ikisisitiza kuwa: Mashambulizi ya kichokozi ya jeshi lenu dhidi ya ardhi na mamlaka ya kujitawala Lebanon hayatapita hivi hivi bila kujibiwa.

Haya yanajiri huku vyombo vya habari vya utawala wa kizayuni vikikiri kuwa jeshi la utawala huo ghasibu liko kwenye mashinikizo ambayo halijawahi kushuhudia kutokana na mashambulio ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kwenye medani ya kaskazini ya vita ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wakati huohuo, vyombo vya habari vya utawala wa kizayuni vimeripoti kuwa, wanajeshi za kizayuni wamefikwa na tukio kubwa katika eneo la kusini mwa Lebanon. Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa, shambulio la Muqawama limelenga moja kwa moja kifaru au gari dogo la kijeshi la utawala wa kizayuni kwenye mpaka wa Lebanon.

Taarifa ya Ijumaa ya Hizbullah imesisitiza kuwa: Hizbullah inaunga mkono umoja wa kitaifa wa Lebanon, mamlaka kamili ya kujitawala na kukomboa ardhi ya nchi, na inapinga aina zote za fitina.