Ayatullah Khatami: Uwezo wa makombora wa Iran umeidhalilisha Marekani
-
Ayatullah Khatami: Uwezo wa makombora wa Iran umeidhalilisha Marekani
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Marekani ilitaka kuangamiza uwezo wa makombora wa Iran, lakini ilishindwa na kuufeli katika mpango wake huo.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya wauumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala yya Ijumaa na kubainisha kwamba, uwezo huo wa makombora wa Iran umeifanya Marekani idhalilike; na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, utaendelea kuifanya idhalilike pia katika siku zijazo.
Akihutubia waumini katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Musalla wa Imam Khomeini Ayatullah Khatami amesema: “Katika zaidi ya siku 160 za mapambano na muqawama, Mwenyezi Mungu amewajaalia wananchi wa Iran neema na msaada mwingi. Miongoni mwao ni kwamba adui alitaka kuuangamiza mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, si kwamba tu alishindwa kuuangamiza mfumo huo, bali Iran leo imekuwa nguvu kubwa duniani.”
Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameeleza kuwa, adui alitaka kuirudisha Iran katika zama za mawe, lakini leo dunia imeelewa kwamba, serikali yenyewe ya Marekani ndiyo iliyo katika fikra za zama za mawe; kwa sababu kimsingi utawala wa Marekani hauujui chochote kuhusu ustaarabu na demokrasia. Kivitendo, wao wenyewe wamegeuka kuwa watu wa zama za mawe.”
Sayyid Ahmad Khatami ameongeza kuwa, “adui alikuwa akilenga kuigawa Iran na kuifanya iwe nchi saba, ili Iran isiendelee kubaki kuwa nchi moja na yenye umoja. Lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, katika vita hii iliyodumu zaidi ya siku 160, hata katika vita vya siku 12, na wala katika vita vya miaka minane, hata shibiri moja ya ardhi ya Iran haikupungua, na katu haitapungua.”
Aidha amesema “Mkuu wa Majeshi ya Marekani na kiongozi mkuu wa vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo alitaka Marekani ijiondoe mara moja katika vita dhidi ya Iran, na akatangaza kwamba matokeo ya vita yalikuwa kinyume na malengo yao. Amekiri wazi kwamba, walianzisha vita, lakini matokeo waliyopata yalikuwa kinyume na walichokusudia.”