Rais wa Belarus: Wairani hawajawahi kumpigia magoti mtu yeyote
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141578-rais_wa_belarus_wairani_hawajawahi_kumpigia_magoti_mtu_yeyote
Rais Alexander Lukashenko wa Belarus amesema kuwa, warithi wa Wairani, watu wa nchi hiyo, hawajawahi kumpigia magoti mtu yeyote. Je, Marekani haifahamu historia hii?”
(last modified 2026-09-20T04:30:45+00:00 )
Sep 20, 2026 04:29 UTC
  • Rais Alexander Lukashenko wa Belarus
    Rais Alexander Lukashenko wa Belarus

Rais Alexander Lukashenko wa Belarus amesema kuwa, warithi wa Wairani, watu wa nchi hiyo, hawajawahi kumpigia magoti mtu yeyote. Je, Marekani haifahamu historia hii?”

Rais wa Belarus amesema hayo akizungumza katika mkutano na kundi la vijana wa nchi hiyo na kueleza kwamba, “Magharibi ilianzisha vita dhidi ya Iran kwa sababu ilikuwa ikilenga kupata utajiri wa nchi hiyo.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Belta, Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, aliendelea kuwaambia vijana wa Belarus:

“Watu wengi walijaribu kututenganisha na Russia mwaka 2020. Kama wangefanikiwa, nasi tungejikuta katika hali kama ya Ukraine. Je, mna uwezo wa kuiongoza nchi na kuilinda? Kama mnao uwezo huo, basi anzeni kazi kesho. Mimi, kwa kadiri iwezekanavyo, nimechoshwa na mamlaka haya na nimeanza kuchoshwa nayo.”

Lukashenko alibainisha kuwa kwa sasa dunia inashuhudia mgawanyo mpya wa nguvu. Alisisitiza kuwa Belarus inapaswa, katika mazingira hayo, kusimama imara na kuwa thabiti kwa kutegemea washirika wake.

Aidha, Lukashenko alisema anaamini kuwa, shinikizo la nchi za Magharibi dhidi ya Belarus linatokana na msimamo wa Wabelarus wa kulinda urithi wao katika nyanja za kiroho, kiutamaduni na kiuchumi.

Wakati huo huo, alisema baadhi ya wachambuzi wa Magharibi huandika kuhusu historia ya Belarus, utambulisho wa nchi hiyo na hisia za asili za kuheshimu wamiliki wa ardhi.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la juhudi za baadhi ya mataifa ya dunia ya kupinga matumizi ya vikwazo vya upande mmoja, shinikizo la kiuchumi na matumizi ya nguvu za kijeshi katika mahusiano ya kimataifa. Kundi la BRICS limeibuka kuwa mojawapo ya majukwaa muhimu katika juhudi hizo, likisisitiza kuheshimiwa mamlaka ya kitaifa, sheria za kimataifa, diplomasia na mfumo wa kimataifa unaoshirikisha mataifa kwa usawa zaidi. Wakati huo huo, baadhi ya nchi hizo zimeongeza ushirikiano wa kiuchumi na kifedha katika jitihada za kupunguza utegemezi wa mifumo inayotawaliwa na mataifa ya Magharibi.