-
Waziri wa Ulinzi: Iran itakuwa na teknolojia ya kisasa zaidi katika vita vyovyote vipya
Sep 14, 2026 04:02Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itakuwa na maendeleo makubwa zaidi ya kiteknolojia iwapo vita vingine vitazuka.
-
Wairani 352,983 washtaki Marekani na Israel kwa vita vya kwanza dhidi ya Iran
Sep 13, 2026 11:18Kesi ya kwanza ya madai iliyofunguliwa na familia za waathiriwa wa “Vita vya Siku 12” vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran mwezi Juni 2025, ilisikilizwa Jumapili asubuhi katika Mahakama ya Iran jijini Tehran.
-
Pakistan: Tunafanya juhudi za kuzirudisha Marekani na Iran kwenye meza ya mazungumzo
Sep 12, 2026 04:23Balozi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amesema: "tunafanya juhudi za kuzirudisha Marekani na Iran kwenye meza ya mazungumzo".
-
Jenerali Mohsen Rezaei: Marekani impokea ‘onyo la wazi’ kutoka kwa makombora mapya ya Iran
Sep 08, 2026 11:24Afisa mkuu wa usalama wa Iran amesema kuwa Marekani imepokea “onyo la wazi” kutokana na uwezo mpya wa makombora wa Jamhuri ya Kiislamu, baada ya Tehran kufanya majaribio ya kombora jipya la kupambana na meli za kivita karibu na meli ya kivita ya Marekani katika maji ya kikanda.
-
Makombora ya Balistiki ya IRGC yalazimisha meli za Kivita za Marekani kutoroka
Sep 06, 2026 04:20Kikosi cha Anga za Juu cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimerusha makombora kadhaa ya balistiki kuelekea kwenye manowari mbili za Marekani ikiwemo ile yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita na kuzilazimu kutoroka. Meli hizo za kivita zilikuwa zikishiriki katika mzingiro haramu wa baharini wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Qalibaf: Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja dhidi ya ubeberu
Sep 03, 2026 03:26Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja kukabiliana na ubeberu.
-
Iran: Baraza la Usalama la UN lilaani shambulio la Marekani lililoua raia kwenye sherehe ya harusi
Sep 03, 2026 03:19Iran imeliitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani shambulio la Marekani lililolenga nyumba ya makazi iliyokuwa ikiandaa sherehe ya harusi kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu, ambalo limesababisha kuuawa shahidi wa raia watano, akiwemo mtoto wa miaka minne, na kuwajeruhi zaidi ya watu 70 wengine.
-
IRGC yaangamiza askari wengi Wamarekani walioko Jordan baada ya US kuua raia wa Iran kwenye sherehe ya harusi
Sep 02, 2026 02:56Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimetekeleza mfululizo wa operesheni kali za kulipiza kisasi ambazo zimehusisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani zilizolenga kambi na maslahi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi kufuatia vitendo vya hivi karibuni vya utawala huo wa kigaidi vya kuanzisha uchokozi usio na sababu, ambao umepelekea kuuawa shahidi raia kadhaa wasio na hatia wa Jamhuri ya Kiislamu akiwemo mtoto mdogo.
-
Pezeshkian: Marekani ilikiuka MoU ya Islamabad, ikahamia kwenye madai ya kuchupa mipaka ndani ya wiki mbili
Sep 01, 2026 14:56Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba usalama endelevu haupatikani kupitia makabiliano, bali kupitia njia ya kuaminiana, kuheshimu mamlaka ya kujitawala ya nchi nyingine, kutoingilia mambo yao ya ndani, na ushirikiano kati ya serikali, na ametoa wito wa kuimarishwa ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi katika Shirika la Ushirikiano la Shanghai.
-
Mshauri wa Trump aliyejiuzulu adai: Marekani inaweza ikaishambulia Iran kwa silaha za nyuklia
Aug 30, 2026 12:17Mshauri wa zamani wa rais wa Marekani wa masuala ya kupambana na ugaidi Joe Kent, amedai kuwa Marekani inaweza ikatumia silaha za nyuklia dhidi ya Iran baada ya kushindwa kuupindua mfumo wa utawala wa Iran kwa kutumia silaha za kawaida.