Spika Qalibaf: Hormuz haitafunguliwa hadi pale Marekani itakapotimiza masharti ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141598-spika_qalibaf_hormuz_haitafunguliwa_hadi_pale_marekani_itakapotimiza_masharti_ya_iran
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema, Mlango-Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa hadi pale Marekani itakapotambua haki za Jamhuri ya Kiislamu na kutimiza masharti yake iliyotoa kwa ajili ya kuhitimishwa vita.
(last modified 2026-10-15T06:24:13+00:00 )
Sep 20, 2026 14:01 UTC
  • Spika Qalibaf: Hormuz haitafunguliwa hadi pale Marekani itakapotimiza masharti ya Iran

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema, Mlango-Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa hadi pale Marekani itakapotambua haki za Jamhuri ya Kiislamu na kutimiza masharti yake iliyotoa kwa ajili ya kuhitimishwa vita.

Qalibaf ametangaza msimamo huo katika kikao cha bunge leo Jumapili, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kujihami Kutakatifu, ambayo ni kumbukumbu ya kuanza kwa vita vya miaka minane vya kulazimishwa, vilivyoanzishwa katika miaka ya 1980 na dikteta wa wakati huo wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya Iran.

"Ujumbe wetu umefikishwa kwa uwazi kwa upande wa pili, na masharti yetu yamefafanuliwa kupitia wapatanishi. Adui anajua vyema kuwa njia ya udanganyifu na kulazimisha mambo kutokea upande mmoja imefungwa," amesisitiza Spika wa Bunge la Iran.

"Bila masharti haya kutimizwa, haki halali za Iran kutambuliwa, na ahadi zilizotolewa na Marekani kutekelezwa, hakutakuwa na matarajio yoyote ya kurejea kwenye utaratibu wa awali wa mazungumzo na kuufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz" ameeleza bayana Spika huyo wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran.

Halikadhalika, Qalibaf ameeleza kwamba, mfumo wa zamani wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi umeshaporomoka, na sasa ni jukumu la nchi za Kiislamu za eneo hilo kuanzisha na kutekeleza mfumo mpya.

Iran iliweka kizuizi cha upitaji vyombo vya majini katika Mlango-Bahari wa Hormuz, -ambayo ni njia muhimu ya kimkakati ya majini inayopitisha sehemu moja ya tano ya mahitaji ya mafuta duniani-, likiwa ni jibu kwa uchokozi haramu wa kijeshi wa Marekani na Israel ulioanza tarehe 28 Februari mwaka huu.

Mnamo tarehe 17 Juni, Tehran na Washington zilitia saini Hati ya Maelewano (MoU) iliyosimamiwa na Pakistan, ambayo katika Ibara yake ya 5 imekabidhi mikononi mwa Iran pekee jukumu la kufungua na kusimamia mlango-bahari huo.

Hata hivyo, Washington ilijaribu kudhoofisha mamlaka ya utawala ya Iran juu ya njia hiyo muhimu ya nishati duniani, ikaanzisha upya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran, na kuweka mzingiro wa majini kinyume na makubaliano ya kuhitimisha vita.

Hatua hizo haramu za Marekani ziliifanya Iran itangaze kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kwa shughuli zote za usafiri…/