Gazeti la kizayuni ladai: Trump amekasirika kwa ahadi alizopewa na Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i142180-gazeti_la_kizayuni_ladai_trump_amekasirika_kwa_ahadi_alizopewa_na_netanyahu
Gazeti moja la Kiebrania katika utawala wa kizayuni wa Israel limedai kuwa rais wa Marekani Donald Trump amemkasirikia na amechukizwa na waziri mkuu wa utawala huo haramu Benjamin Netanyahu.
(last modified 2026-10-14T10:25:58+00:00 )
Oct 14, 2026 10:23 UTC
  • Gazeti la kizayuni ladai: Trump amekasirika kwa ahadi alizopewa na Netanyahu

Gazeti moja la Kiebrania katika utawala wa kizayuni wa Israel limedai kuwa rais wa Marekani Donald Trump amemkasirikia na amechukizwa na waziri mkuu wa utawala huo haramu Benjamin Netanyahu.

Yedioth Ahronoth limeandika, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amempoteza Trump, na utawala huo umeipoteza Marekani.

Gazeti hilo limeeleza katika ripoti yake: "huku tarehe ya uchaguzi wa bunge wa Israel Ahronoth ikikaribia, Netanyahu hajapokea ishara zozote za kisiasa alizokuwa akizitafuta kutoka Ikulu ya White House".

Yedioth Ahronoth, limenukuu chanzo kilicho karibu na Trump na kudai kwamba rais huyo wa Marekani amemkasirikia Netanyahu kwa kutomaliza vita vya Ghaza, kwa sababu kufanya hivyo kumezuia kupigwa hatua katika mkataba wa Abraham wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na tawala za nchi za Kiarabu.

Sababu nyingine ya hasira ya Trump dhidi ya Netanyahu kulingana na ripoti ya gazeti hilo la Kiebrania, ni ahadi zake za kupatikana ushindi wa haraka katika vita vya kichokozi, vilivyoanzishwa kwa pamoja na Washington na Tel Aviv dhidi ya Iran.

Yedioth Ahronoth limeongeza kuwa, juhudi za baraza la mawaziri la Netanyahu za kupata uungaji mkono wa hadharani kutoka Ikulu ya White House hadi sasa hazijazaa matunda.

Hii ni katika hali ambayo, sera zote za kushupalia kivita za utawala wa Kizayuni kuhusiana na eneo la Asia Magharibi na uchokozi wa kijeshi ulioanzishwa na Washington na Tel Aviv vimefanywa kwa uratibu wa pamoja wa pande hizo mbili…/