Mripuko waangamiza na kujeruhi Wazayuni 20 Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i142146-mripuko_waangamiza_na_kujeruhi_wazayuni_20_palestina
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kutokea mripuko mkubwa katika eneo la al Khalil, kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kupelekea kuangamizwa na kujeruhiwa Wazayuni wasiopungua 20.
(last modified 2026-10-13T03:44:10+00:00 )
Oct 13, 2026 03:35 UTC
  • Mripuko waangamiza na kujeruhi Wazayuni 20 Palestina
    Mripuko waangamiza na kujeruhi Wazayuni 20 Palestina

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kutokea mripuko mkubwa katika eneo la al Khalil, kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kupelekea kuangamizwa na kujeruhiwa Wazayuni wasiopungua 20.

Shirika la Habari la Mehr limenukuu duru za Kizayuni zikidhibitisha habari hiyo na kutangaza kuwa kuna idadi kubwa ya Wazayuni waliojeruhiwa katika mripuko huo.

Kituo cha televisheni cha Channel 12 cha Israel kimetangaza kuwa kwa uchache Mzayuni mmoja ameangamizwa na wengine wasiopungua 19 wamejeruhiwa kikibainisha kuwa watatu kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya sana.

Wakati huo huo, gazeti la Kizayuni la "Maariv" limeripoti kuwa mripuko huo umetokea kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na hadi wakati linaandika habari hiyo, hali ilikuwa bado ni tete na shughuli za uokoaji zilikuwa zinaendelea.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa mwanafunzi mmoja aligusa kitu kilichokuwa na miripuko na huenda alikuwa amekibeba kwenye begi lake kabla ya mripuko huo.

Hata hivyo, polisi katika kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kiryat Shmona wamesema kuwa bado hawana uhakika kama mripuko huo umesababishwa na bomu au kichwa cha kombora ambacho hakikuripuka wakati wa vita.

Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa, helikopta imetumwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya kusafirisha majeruhi.

Kwa upande wake gazeti jingine la Kizayuni la "Israel Hayom" limeripoti kuwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu alisitisha matangazo ya moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii yaliyohusu uchaguzi baada ya kutokea mripuko huo.

Redio ya Jeshi la Israel imetangaza kuwa watu 20 walijeruhiwa katika tukio hilo la al Khalil; watatu wakiwa katika hali mahututi.

Wizara ya Elimu ya Israel imesema: Hilo ni tukio hatari sana, na kwamba ilikuwa inashirikiana na pande husika kuwasaidia wanafunzi, wafanyakazi na familia zao.