Kiongozi mmoja wa Ulaya: Vikwazo vimeshindwa kuzuia ustawi na maendeleo ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i142176-kiongozi_mmoja_wa_ulaya_vikwazo_vimeshindwa_kuzuia_ustawi_na_maendeleo_ya_iran
Kiongozi mmoja wa Ulaya amekiri kuwa Iran imeendelea kupiga hatua za kimaendeleo licha ya kuwekewa vikwazo vingi. Hii ikiwa na maana kwamba vikwazo vimeshindwa kulizuia taifa la Iran kupata ustawi na maendeleo.
(last modified 2026-10-14T03:28:43+00:00 )
Oct 14, 2026 03:27 UTC
  • Kiongozi mmoja wa Ulaya: Vikwazo vimeshindwa kuzuia ustawi na maendeleo ya Iran

Kiongozi mmoja wa Ulaya amekiri kuwa Iran imeendelea kupiga hatua za kimaendeleo licha ya kuwekewa vikwazo vingi. Hii ikiwa na maana kwamba vikwazo vimeshindwa kulizuia taifa la Iran kupata ustawi na maendeleo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, David O'Sullivan, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya vikwazo, alikiri kuwa sera ya vikwazo ya Umoja wa Ulaya ina mapungufu yake ya dhati na haihakikishi kufikiwa malengo yaliyokusudiwa.

"Nadhani tunapaswa kuelewa kuwa vikwazo siku zote huwa na mapungufu yake," amesema O'Sullivan.

Ametoa mifano ya Korea Kaskazini na Iran, nchi ambazo zimeendelea kupiga hatua kimaendeleo licha ya kuwekewa vikwazo vingi vya kila upande.

Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Ulaya amekiri pia kuwa vikwazo vilivyowekwa vya kuzibana nchi hizo zisipate ustawi na maendeleo ya teknolojia muhimu, si lazima vizuie kuenea teknolojia hizo na kufikiwa maendeleo makubwa zaidi.

Kwa mujibu wa O'Sullivan, maendeleo ya kiteknolojia yamefanya utekelezaji wa vikwazo na udhibiti wa mauzo ya nje kuwa mgumu zaidi. Maendeleo hayo yanapunguza uwezo wa nchi zilizoweka vikwazo kudhibiti kikamilifu usambazaji wa bidhaa na teknolojia. 

Matamshi hayo ya afisa huyo wa ngazi za juu wa Ulaya yamekuja katika hali ambayo, Kazem Gharibabadi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa amesema kuwa Iran iko tayari kwa hali yoyote ile, akisisitiza kuwa, "Tuko tayari kwa diplomasia pamoja na vita kwa lengo la kulinda usalama wa nchi yetu."

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Araby, Kazem Gharibabadi amesema, Tehran inakamilisha majibu yake kuhusiana na maoni na mitazamo ya upande wa Marekani kuhusu pendekezo ambalo Iran ililiwasilisha hivi karibuni mjini New York.

Akiashiria mchakato wa mazungumzo ya Iran na Marekani, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika Mazungumzo ya Islamabad huku Marekani ukikiuka waziwazi wajibu wake kuhusu makubaliano hayo.