-
IRGC yajibu mapigo kwa madai ya US kuhusu udhibiti wa Hormuz: Tieni mguu ugani mjionee wenyewe
Oct 14, 2026 10:39Kamanda wa Vikosi vya Wanamaji vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amekanusha vikali madai ya Marekani kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz uko wazi na unadhibitiwa na Washington, huku akiwataka wanajeshi wa Marekani wasogee karibu zaidi kama wanataka kufahamu ni nani hasa anayeidhibiti njia hiyo muhimu ya majini.
-
Wabunge 77 wa US waitaka serikali na Pentagon zitoe maelezo kuhusu mauaji ya raia wa Iran
Oct 14, 2026 10:32Wabunge 77 wa Marekani wameandika barua wakitaka maelezo kutoka kwa serikali na wizara ya vita ya nchi hiyo Pentagon kuhusu mashambulizi dhidi ya raia katika vita dhidi ya Iran na vifo vya baadhi ya raia hao.
-
Gazeti la kizayuni ladai: Trump amekasirika kwa ahadi alizopewa na Netanyahu
Oct 14, 2026 10:23Gazeti moja la Kiebrania katika utawala wa kizayuni wa Israel limedai kuwa rais wa Marekani Donald Trump amemkasirikia na amechukizwa na waziri mkuu wa utawala huo haramu Benjamin Netanyahu.
-
Baqaei: Kimya cha Ulaya kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya ICC ni shambulio dhidi ya sheria na haki
Oct 12, 2026 03:20Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kutokuchukua hatua na ukimya wa nchi za Ulaya kuhusu vikwazo vya Marekani dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), pamoja na vitisho vya kuifuta mahakama hiyo, ni sawa na kushiriki katika mashambulizi dhidi ya sheria na haki.
-
Mawakili wa Ulaya, US wajiunga na kampeni ya kuishtaki Washington kwa mauaji ya watoto 168 wa Minab
Oct 11, 2026 11:57Idadi ya wanasheria wa kigeni kutoka Ulaya na hata ndani ya Marekani wanaojitolea kushiriki katika ufunguaji kesi dhidi ya Washington kuhusiana na mauaji ya halaiki ya watoto 168 wa skuli ya Minab inazidi kuongezeka na kutoa msukumo kwa juhudi za Iran za kuhakikisha Marekani inawajibishwa kwa jinai yake hiyo.
-
Meja Jenerali Vahidi: Tutajibu kwa nguvu kila tishio katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Oct 09, 2026 09:52Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), ametoa onyo akisema kuwa jeshi hilo liko tayari kutoa jibu kali kwa hatua yoyote ya kimakosa ya adui katika kufanya mahesabu yake.
-
Abbas Araghchi: Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) haiwezi kuwahadaa watu milele
Oct 09, 2026 02:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameikosoa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, kwa kuficha taarifa kuhusu hasara iliyolipata jeshi la Marekani na kusisitiza kwamba, hamuwezi kuwahaada watu mielele.
-
Muqtada Sadr aionya Marekani kuhusu kuingilia kati mambo ya ndani ya Iraq
Oct 09, 2026 02:44Sayyid Muqtada Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq amesisitiza umuhimu wa uhuru na mamlaka ya kujitawala nchi hiyo na ameionya Marekani dhidi ya kuendelea na harakati zake zenye madhara na za kuingilia mambo ya ndani ya Iraq. Muqtada Sadr amebainisha kuwa, Wairaqi watasimama dhidi ya kila aina ya uvamizi.
-
Uchaguzi wa urais Brazil waingia duru ya pili, Polisi yachunguza madai kuhusu uingiliaji wa Marekani
Oct 05, 2026 10:43Uchaguzi wa urais nchini Brazil umeingia katika duru ya pili, huku kura za wapigakura walioacha kura tupu, walioharibu kura zao, na za wafuasi wa wagombea walioshindwa, zikitarajiwa kuwa ndizo zitakazoainishia mshindi rasmi wa uchaguzi huo.
-
Hizbullah ya Lebanon: Kufukuzwa Marekani nchini Iraq ni mwanzo wa mwisho wa uwepo wa kijeshi wa Washington Asia Magharibi
Oct 03, 2026 02:55Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, imesema katika taarifa yake kwamba, kufukuzwa majeshi ya Marekani kutoka katika ardhi ya Iraq ni mafanikio ya kihistoria na ushindi mkubwa.