Nini maana ya Marekani kushindwa kistratejia?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137256-nini_maana_ya_marekani_kushindwa_kistratejia
Kwa nini Marekani inakaribia kushindwa kistratejia? Jibu la swali hili linapatika katika utambulisho wa vita vya sasa vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-03-09T13:36:04+00:00 )
Mar 09, 2026 12:32 UTC
  • Nini maana ya Marekani kushindwa kistratejia?

Kwa nini Marekani inakaribia kushindwa kistratejia? Jibu la swali hili linapatika katika utambulisho wa vita vya sasa vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mapigano kama haya, ushindi haupatikani tu kwa kupiga shabaha au kufanya mashambulizi kadhaa, bali hupatikana pale unapoweza kuulazimisha upande wa pili kusimamisha kabisa mapigano yake.

Hili ndilo tatizo hasa la Marekani. Iran imeonyesha kwamba inaweza kudumisha uwezo wake wa kutoa mapigo hata inapokuwa chini ya mashinikizo ya mashambulizi; iwe ni kupitia makombora na ndege zisizo na rubani, au kwa kufunga njia muhimu za usafirishaji nishati kama vile Lango-Bahari la Hormuz.

Kwa hoja hiyo, baadhi ya wachambuzi wa nchi za Magharibi wanasema, iwapo Iran itaweza kurefusha muda wa mapigano haya na bado ikawa na uwezo wa kujibu mapigo, kwa hakika itakuwa imezuia Marekani kufikia lengo lake kuu.

Kwa upande mwingine, vita vya muda mrefu si suala la kijeshi tu. Kuvurugwa mauzo ya nje ya nishati, kupanda bei, migogoro katika mnyororo wa usambazaji wa bidhaa na shinikizo la kiuchumi duniani ni mambo yanayoweza kusababisha gharama kubwa za kisiasa kwa serikali ya Marekani na washirika wake.

Katika hali kama hii, machaguo ya kijeshi sio rahisi sana. Vilevile,kuwaua viongozi wa kisiasa si lazima kupelekee nchi kuporomoka.

Kwa upande mwingine, vita vya nchi kavu katika nchi yenye ukubwa wa Iran vinahitaji mamia ya maelfu ya wanajeshi. Na hata kuteka maeneo nyeti ya kiuchumi bila kufuta kabisa uwezo wa makombora wa Iran kutakuwa na gharama kubwa sana. Ndiyo maana baadhi ya wachambuzi wakasema kuwa suala la msingi si nani anayefanya mashambulizi mangapi; bali ni nani anayeweza kumudu vita vya kuuchosha upande wa pili.

Na katika hali kama hii, ikiwa upande wa pili utashindwa kuvunja irada na azma ya nchi nyingine, hata nguvu kubwa zaidi za kijeshi zinaweza kushindwa kufikia malengo zinayofuatilia. Hili ndilo jambo linaloitwa katika fasihi ya kimkakati kwamba ni: Kushindwa Kistratejia.