Muirani anyongwa kwa kuwagonga polisi wakati wa ghasia zilizofadhiliwa na wageni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140714-muirani_anyongwa_kwa_kuwagonga_polisi_wakati_wa_ghasia_zilizofadhiliwa_na_wageni
Mwanamume aliyehukumiwa kwa kuwagonga na kuwajeruhi maafisa kadhaa wa polisi wakati wa ghasia zilizoungwa mkono na kufadhiliwa na wageni kote Iran mwezi Januari, ameuawa.
(last modified 2026-08-16T09:19:43+00:00 )
Aug 16, 2026 09:17 UTC
  • Shahram Sadeghi
    Shahram Sadeghi

Mwanamume aliyehukumiwa kwa kuwagonga na kuwajeruhi maafisa kadhaa wa polisi wakati wa ghasia zilizoungwa mkono na kufadhiliwa na wageni kote Iran mwezi Januari, ameuawa.

Shirika la habari la Mizanonline la Mahakama limeripoti kwamba mtu huyo, aliyetambuliwa kwa jina la Shahram Sadeghi, amenyongwa mapema leo Jumapili.

Hukumu yake ya kifo na kunyang'anywa mali, ilizotolewa na Mahakama ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Karaj kwa mashtaka ya "kuchukua hatua za kiutendaji kwa niaba ya utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na makundi ya uadui," ilithibitishwa na Mahakama Kuu ya Iran.

Tarehe 8 Januari mwaka huu, Sadeghi aliwagonga polisi kwa makusudi kwa gari lake kwa kasi kubwa karibu na makutano ya Golzar huko Karaj, magharibi mwa Tehran, na kuwajeruhi saba kati yao kichwani, miguuni na mikononi, na kumwacha mmoja akiwa amepoteza fahamu kwa miezi mitatu.

Baada ya shambulio hilo la kikatili, Shahram Sadeghi alikimbia eneo la tukio baada ya kuchoma moto gari lake mwenyewe. Baadaye alipatikana katika maficho yake katika kituo cha kurekebisha tabia ya waraibu wa dawa za kulevya.

Baada ya uchunguzi kukamilika na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka, mashtaka yaliwasilishwa dhidi ya Sadeghi, ambaye kesi yake ilisikilizwa na Mahakama ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Karaj mbele ya wakili wake.

Makundi ya watu waliokuwa na silaha na magaidi wanaoungwa mkono na kufadhiliwa na wageni waliteka nyara maandamano ya amani kuhusu malalamiko ya kiuchumi kote Iran mnamo Januari 8 na 9, na kusababisha uharibifu mkubwa wa maduka, taasisi za serikali na vifaa vya huduma za umma, na kuua au kujeruhi maelfu ya watu.

Mamlaka za Iran zimethibitisha kwamba mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel yalihusika moja kwa moja, yakitoa ufadhili, mafunzo na msaada wa vyombo vya habari kwa wahusika.