Baghaei amjibu Waziri Mkuu wa Canada kuhusu uchochezi wa Vita wa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141688-baghaei_amjibu_waziri_mkuu_wa_canada_kuhusu_uchochezi_wa_vita_wa_trump
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Badala ya Waziri Mkuu wa Canada kulaani uchokozi na uchochezi wa vita wa Marekani, amejaribu kuhalalisha vitendo hivyo, akielezea tishio la kuangamizwa nchi kama "maneno tu ya wakati wa vita".
(last modified 2026-09-24T12:05:51+00:00 )
Sep 24, 2026 12:04 UTC
  • Baghaei amjibu Waziri Mkuu wa Canada kuhusu uchochezi wa Vita wa Trump

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Badala ya Waziri Mkuu wa Canada kulaani uchokozi na uchochezi wa vita wa Marekani, amejaribu kuhalalisha vitendo hivyo, akielezea tishio la kuangamizwa nchi kama "maneno tu ya wakati wa vita".

Esmaeil Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amejibu kupitia ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii matamshi yaliyotolewa na Mark Carney, Waziri Mkuu wa Canada, ambaye amejaribu kuhalalisha uchokozi wa kijeshi na kauli za kuchochea vita za Rais wa Marekani dhidi ya Iran. Ameandika: Mark Carney anapaswa kutambua kuwa wakati hauruhusu kudumu kwa muda usio na kikomo udanganyifu na unafiki.

Amesema: "Utafika wakati ambapo wale waliojificha nyuma ya kivuli cha vitisho na ubabe wa Marekani, wakidhani kuwa kwa kukariri lugha ya wenye nguvu wataweza kujikinga na madhara ya siasa za mabavu, watathibitishiwa kuwa kupuuza ukweli na kukanyaga heshima na hadhi binafsi hakuleti kinga yoyote; bali humuacha mtu akiwa hana ulinzi wowote na kutegemea tu huruma ya mbabe huyo anayetumia mabavu."

Ameongeza: "Huenda siku hiyo, wataitazama Iran ya leo na kutambua kuwa nchi ileile ambayo waliungana na wababe katika kujaribu kuivunja, ndiyo iliyofanikiwa - kwa kusimama imara dhidi ya vitisho na mashinikizo - kuendeleza mwenge wa matumaini, ambao, kama ungezimwa, ungeipa fursa nguvu ya kibeberu na kibabe kutawala wananadamu, na hivyo kupelekea ustaarabu wa mwanadamu wa kutatua migogoro kuzikwa chini ya mantiki katili ya mabavu."