Kwa nini fikra ya "Ulinzi" inasalia kuwa takatifu kwa Wairani?
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141736-kwa_nini_fikra_ya_ulinzi_inasalia_kuwa_takatifu_kwa_wairani
Kwa Waajemi au Wairani, "Ulinzi Mtakatifu" si simulizi ya vita pekee, bali ni fikra iliyokita mizizi katika utambulisho na utamaduni, ikithibisha uzoefu wa mapambano, kujitegemea, umoja wa kitaifa na muqawama dhidi ya vitisho vya nje.
(last modified 2026-09-26T06:32:00+00:00 )
Sep 26, 2026 06:25 UTC
  • Kwa nini fikra ya

Kwa Waajemi au Wairani, "Ulinzi Mtakatifu" si simulizi ya vita pekee, bali ni fikra iliyokita mizizi katika utambulisho na utamaduni, ikithibisha uzoefu wa mapambano, kujitegemea, umoja wa kitaifa na muqawama dhidi ya vitisho vya nje.

Kwa Wairani, "Wiki ya Ulinzi Mtakatifu" huadhimisha mapambano ya vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa Ba'ath wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Karibu miongo minne baada ya kumalizika vita hivyo, ulinzi huo bado unaendelea, ambapo sasa fikra hiyo inaheshimiwa na kuenziwa zaidi kuliko miaka ya huko nyuma.

Ulinzi Mtakatifu wakati wa vita hivyo vya kulazimishwa vya miaka minane ulileta mafanikio makubwa ambapo mkakati wa "uzuiaji hujuma wa ndani ya nchi" (indigenous deterrence), umejikita moja kwa moja katika uzoefu na changamoto za kipindi cha Ulinzi Mtakatifu au kwa ibara nyingine Kujitetea Kutakatifu. Fikra ya "Muqawama", ambayo leo hii ndio msingi mkuu wa sera za kigeni za Iran katika eneo, ilitokana na uzoefu wa kipindi cha "Ulinzi Mtakatifu" (Sacred Defense). Uwezo wa Iran wa "kukabiliana na mazingira magumu" pia unatokana moja kwa moja na uzoefu wa kuendesha vita hivyo vya miaka minane.

Wakati huo huo, Ulinzi Mtakatifu uliweka msingi wa "mtazamo wa kiutamaduni" ambao bado ni muhimu sana kwa jamii na mfumo wa kisiasa. Utamaduni wa "kujitolea mhanga" na "kutokuwa na hofu mbele ya adui" umegeuka kuwa thamani ya pamoja miongoni mwa wananchi wa Iran. Ulinzi Mtakatifu uliifundisha Iran kwamba, katika ulimwengu uliojaa vitisho na unaotawaliwa na madola yenye kiburi yanayotumia mabavu na ukandamizaji, kufikia hatua ya "kujitegemea kimkakati," "uwezo wa kuzuia uchokozi wa adui," na "mshikamano wa kiutamaduni dhidi ya hujuma za nje" kunaweza kuiletea nchi usalama na nguvu ya kutegemewa wakati wa kukabiliana na vitisho vya nje.

Moja ya mafanikio makubwa zaidi ya "Ulinzi Mtakatifu" wa miaka minane, ni kuvunjwa kwa nadharia ya "kutegemea zana na silaha za kigeni." Hili lilifungua njia kwa ajili ya kustawi kwa viwanda vya ndani katika sekta ya ulinzi, viwanda ambavyo leo hii vimepelekea kushindwa kwa maadui wa Marekani na Wazayuni.

Vita vya miaka minane vya Kujitetea Kutakatifu kilikuwa kipindi ambapo tofauti za kisiasa na kimatabaka ziliwekwa kando mbele ya vitisho vya nje, na "umoja wa kitaifa" ukaimarishwa miongoni mwa Wairani. Hata leo, ambapo adui alitarajia kutokea mpasuko na mgawanyiko kati ya wananchi na mfumo wa utawala, umma umeendelea kudumisha umoja wake mbele ya vitisho vya nje. Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi aliyeuawa shahidi na magaidi wa Marekani na Wazayuni aliutaja umoja huu kama "muungano mtakatifu", fikra iliyokusudiwa kuvunja tamaa ya adui na kuiongoza Iran kuelekea ushindi katika kipindi hiki kigumu.

Ulinzi umekuwa mgumu na tata zaidi katika mazingira ya sasa, kwani adui sasa anatumia rasilimali na nguvu zake zote kupinga uwepo wa Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Mbali na kuwaua kigaidi viongozi wakuu wa kisiasa, kijeshi na kisayansi, adui anatumia mbinu za kisasa za vita vya kisaikolojia na ushawishi wa kimtazamo (cognitive warfare) katika jaribio la kugeuza maoni ya umma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, jaribio ambalo limeshindwa, kama inavyothibitishwa wazi na mikusanyiko na uwepo mkubwa wa wananchi mitaani kote nchini kwa zaidi ya usiku 200 sasa. Wakati "Ulinzi Mtakatifu" wa miaka minane ukifafanuliwa kama ulinzi wa ardhi na mipaka, "Ulinzi Mtakatifu" dhidi ya vita vya hivi karibuni vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel unapasa kufafanuliwa kama ulinzi wa mamlaka, utambulisho na ustaarabu wa Iran na Uislamu. Kupitia vita hivi, wananchi wa Iran wanajiona kama sehemu ya mfululizo wa mashujaa ambao hawajawahi kusalimu amri mbele ya ukoloni na uchokozi wa maadui.