Majasusi wa US: Haiyumkiniki kubadilisha mfumo wa uongozi Iran
Baraza la Ujasusi la Marekani limesema katika tathmini yake 'ya siri' kwamba, ni muhali kubadilisha mfumo uliokita mizizi wa kisiasa na kiusalama nchini Iran, hata kwa kutumia mashambulizi makali ya kijeshi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Gazeti la Washington Post limenukuu maafisa wenye ufahamu juu ya suala hilo wakikiri kuwa, mfumo wa uongozi wa Iran ni imara na madhubuti, kiasi kwamba hauwezi kutetereshwa na hata mashinikizo makubwa ya kijeshi.
Ripoti hiyo ya tathmini ya Baraza la Ujasusi la Marekani inaacha masuali mengine yasiyo na majibu, kuhusu stratejia inayotumiwa na Rais Donald Trump ambaye amekuwa akikariri mara kwa mara kuwa anataka 'kusafisha' mfumo wa uongozi wa Iran.
Wachambuzi wa mambo wamesema katika ripoti hiyo kuwa, hata baada ya kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, mfumo wa uongozi nchini Iran utaendelea kufanya kazi kupitia mihimili thabiti ya utawala iliyopo.
Haya yanajiiri huku wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wakidokeza kuwa, mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya unakaribia kukamilika. Baraza hilo la kumchagua Kiongozi Mkuu hivi sasa linatekeleza jukumu lililokabidhiwa ili kuweza kumtangaza haraka iwezekanavyo Kiongozi Mkuu mpya kwa mujibu wa Msingi wa 11 wa Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu.
Ikumbwe kuwa, tawala fisadi na dhalimu za Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi haramu na ya kichokozi dhidi ya Iran kuanzia asubuhi ya Jumamosi, Februari 28.
Katika kujibu uchokozi huo wa Marekani na Israel, ambao ulisababisha kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na makamanda kadhaa wakuu wa kijeshi na mamia ya raia wakiwemo watoto wa shule, Iran ilianzisha Operesheni ya Ahadi ya Kweli 4, ikifanya wimbi la mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya shabaha za Israel na kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.