Na’im Qassem: Kukabiliana na utawala wa Israel kunawezekana tu kupitia muqawama
-
Sheikh Na’im Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon
Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, kukabiliana na ubeberu na utawala wa Israel kunawezekana tu kupitia muqawama na mapambano.
Sheikh Na’im Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema hayo katika ujumbe wa video alioutuma kwenye Mkutano wa Shahidi wa Muqawama, uliofanyika kwa mnasaba wa kutimia miaka 55 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wanachuo wa Imamiya nchini Pakistan.
Sheikh Na'im Qassem amesema kuwa muqawama ndiyo njia pekee ya kuikomboa ardhi. Amesisitiza kwamba kukabiliana na ubeberu na utawala haramu wa Israel kunawezekana tu kupitia njia ya muqawama na mapambano.
Kiongozi huyo wa Hizbullah ya Lebaanon amesisitiza kwamba, licha ya kutokuwepo kwa uwiano wa nguvu, chaguo la muqawama limethibitisha ufanisi wake nchini Lebanon. Ameongeza kuwa uzoefu wa muqawama nchini Lebanon umeonyesha kuwa muqawama huikomboa ardhi na wananchi, humlazimisha adui Mzayuni kuondoka akiwa ameshindwa na kudhalilika, na kurejesha suala la Palestina katika uhai na uwezo wake.
Katibu Mkuu huyo wa Hizbullah amelieleza suala la Palestina kuwa suala la msingi, na kusisitiza kwamba muqawama ni jambo la lazima katika aina zake zote.
Akizungumzia vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kkiislamu ya Iran, Sheikh Na’im Qassem amesema: “Uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ulifanywa kwa lengo la kuuangusha mfumo wa Kiislamu unaotawala nchini Iran, lakini mambo yakawa kinyume kwani, kilichojitokeza ni Iran kuibuka mshindi katikka vita hivyo na maadui kushindwa kufikia hata lengo lao moja katika njama zao.