Mwigizaji wa Hollywood: Trump ni gaidi na mhalifu
Mwigizaji maarufu wa Marekani Morgan Freeman ameandika katika ukurasa wake binafsi kwenye mitandao ya kijamii kwamba rais Donald Trump ni gaidi, mbaguzi wa rangi na mhalifu, na kwamba Ikulu ya White House inapaswa kuhesabiwa kuwa ni shirika la kigaidi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, Morgan Freeman, mwigizaji maarufu wa Marekani, aliandika katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kwamba Trump ni gaidi, mbaguzi wa rangi, mtu mwongo na mhalifu.
Akiashiria pia kwamba “Trump si rais wangu,” ametangaza kuwa White House ni shirika la kigaidi.
Hapo awali pia, Jürgen Todenhöfer, mwanahabari na mbunge wa zamani wa Bunge la Ujerumani, alikosoa uungaji mkono wa Kansela wa nchi hiyo kwa Tel Aviv na Washington katika uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kumwambia: “Bw. Merz, acheni kushirikiana na wauaji na simamisheni msaada wa silaha kwa pande hizi mbili.”
Ameandika katika mtandao wa kijamii wa X: “Bw. Friedrich Merz, zuieni Marekani kutumia kambi ya kijeshi ya Ramstein kwa ajili ya mashambulizi haramu dhidi ya Iran, na simamisheni misaada ya kijeshi kwa Tel Aviv na Washington.”
Ameendelea kusema: “Wahalifu wawili mashuhuri wa vita wanaiharibu dunia; hamstahili kuwaunga mkono. Sisi si washirika wenu katika uhalifu.”
Mwanasiasa huyo wa Ujerumani hapo awali pia, akijibu uhalifu wa Marekani katika shambulio dhidi ya shule ya Shajarat Tayyiba mjini Minab, kusini mwa Iran amesema: “Donald Trump (rais wa Marekani) amepoteza ustahiki wa kimaadili katika vita dhidi ya Iran. Sio tu kwamba alisababisha kuuawa kwa wasichana wanafunzi 165, bali pia nchi za Ghuba ya Uajemi zinawaka moto kutokana na hatua zake.”