Waziri Mkuu wa Italia amwambia Trump: Pilipili usioila inakuwashia nini?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i139342-waziri_mkuu_wa_italia_amwambia_trump_pilipili_usioila_inakuwashia_nini
Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni amemshauri Rais wa Marekani, Donald Trump kujalia ya kwake mwenyewe badala na kufuatilia ya wengine baada ya kudai kwamba kiongozi huyo wa Italia anajaribu kuongeza umaarufu na viwango vyake vya kukubalika ndani ya nchi kwa kurekebisha uhusiano na Washington.
(last modified 2026-06-22T14:11:41+00:00 )
Jun 22, 2026 14:09 UTC
  • Meloni amwambia Trump: Pilipili usioila inakuwashia nini?
    Meloni amwambia Trump: Pilipili usioila inakuwashia nini?

Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni amemshauri Rais wa Marekani, Donald Trump kujalia ya kwake mwenyewe badala na kufuatilia ya wengine baada ya kudai kwamba kiongozi huyo wa Italia anajaribu kuongeza umaarufu na viwango vyake vya kukubalika ndani ya nchi kwa kurekebisha uhusiano na Washington.

Ijumaa iliyopita kiongozi huyo wa Italia alimtaja Donald Trump kuwa muongo na kidhabu kwa madai yake kwamba Giorgia Meloni "amemuomba" apige picha naye wakati wa mkutano wa kilele wa G7 uliofanyika nchini Ufaransa.

Siku ya Jumamosi, Trump alikariri madai hayo, akiandika vibaya jina lake kama "Gigiorgia" huku akichapisha kwenye jukwaa lake la Truth Social kwamba " Meloni anataka kufufua urafiki wao ili kuongeza idadi ya wafuasi wake."

Meloni alijibu kwa kuchapisha ujumbe kwenye Instagram kwa luugha ya Kiingereza kwamba: "Rais Trump, mashambulizi haya yanayoendelea bila sababu ya maana hayana mantiki."

"Umaarufu wangu haukuhusu," ameendelea kusema Waziri Mkuu wa Italia na kuongeza: "Ninapendekeza ujishughulishe na mambo yako mwenyewe."

Giorgia Meloni ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Italia alimwambia Trump siku ya Jumamosi kwamba "kuwa rafiki yake hajakusaidia" kupandisha umaarufu wake.

Tangu uliposhika madaraka mwaka wa 2022, utawala wa Meloni umepata ongezeko la viwango vya uungaji mkono wa umma baada ya kushuka mara kwa mara mwaka wa 2025.

Siku ya Jumapili, Trump alieleza kutoridhika kwake na Meloni kwa kukataa kutimiza maombi ya Marekani na kushirikiana na Washington katika vita vyake dhidi ya Iran.

Giorgia Meloni alijibu kwa kusema: "Maadamu mimi ni Waziri Mkuu, Italia inasalia kuwa taifa huru."