SEPAH: "Sayyid wa Muqawama" bado yuko hai na njia yake inaendelea
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) limetoa taarifa maalumu kwa mnasaba wa hauli na kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kussema: "Sayyid wa Muqawama bado yuko hai na njia yake inaendelea kwa utukufu na nguvu kuu."
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imetolewa leo Jumatatu ikiitaja njia ya "Sayyid wa Muqawama" kuwa ni ya kudumu milele.
Taarifa hiyo imesema, damu ya Sayyid Hassan Nasrullah ni chemchemu inayobubujika kwa nguvu ndani ya mwili wa Kambi ya Muqawama, imeinua heshima na fakhari za Hizbullah na Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema: "Sayyid Hassan Nasrullah hakuwa kiongozi tu; bali alikuwa mbunifu wa kimkakati wa Muqawama, mtaalamu wa mikakati katika nyanja za kijeshi na kidiplomasia kama ambavyo pia alikuwa ni kielelezo halisi cha uhusiano usiovunjika kati ya mataifa ya wanamapambano ya eneo hili. Alikifuata vizuri kigezo na ruwaza yake yaani Imam Khamenei (quddisa sirruh) na kuuinua Muqawama kutoka kuwa mbinu tu na kuufanya kuwa mfumo mpana wa kiakili wenye utambulisho na ustaarabu mkubwa.
Vilevile taarifa hiyo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) imesema: "Tab'an, njia ya shahid Sayyid Hassan Nasrullah itaendelezwa na wanamapambano wa Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon na Hizbullah — chini ya uongozi wa mrithi wake stahiki, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sheikh Naim Qassem kwa utukufu, heshima na nguvu kubwa.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) pia limetangaza kuwa: Kuunga mkono Muungano wa Mapambano, kutetea haki za waliokandamizwa na kusimama imara hadi kukombolewa kikamilifu Quds Tukufu, ni wajibu wa kudumu, wa kitaifa na wa kibinadamu wa jeshi hilo.