Netanyahu yuko wapi? Galloway ashangazwa na video yake ya Akili Mnemba
Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi Uingereza, George Galloway amesema video ya hotuba ya Benjamin Netanyahu iliyotengezwa kwa kutumia Akili Mnemba (AI) inaibua masuali mengi kuhusu kitendawili cha aliko Waziri Mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Galloway amesema video hiyo ya AI iliyogubikwa na kasoro nyingi ikiwemo Netanyahu akiwa na vidole sita imeibua masuali mengi bila majibu, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu nduli huyo wa vita wa Israel.
Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa X kuhusu video hiyo bandia ya Netanyahu, Galloway ambaye amewahi kuwa Mbunge katika Bunge la Uingereza ameandika: Je hili limefanyika kweli? Kwa nini Israel ilisambaza hotuba ya Akili Mnemba ya Netanyahu usiku uliopita, ambapo Waziri Mkuu huyo ameonekana dhahiri akiwa na vidole sita? Yuko wapi (Netanyahu)? Yuko wapi Ben Gvir?
Galloway ameshangazwa pia na hatua ya vyombo vya habari vya Magharibi ya kufumbia macho video hiyo bandia ya Netanyahu na kutouliza masuali mazito kuhusu aliko mtawala huyo wa Israel.
Netanyahu hajaonekana hadharani wala kusambaza hotuba zake za video kwa siku kadhaa sasa, tangu vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viliposhadidisha mashambulizi ya kulipiza ya kisasi ya Ahadi ya Kweli ya 4.
Siku chache zilizopita, uvumi ulienea kwenye mitandao ya kijamii kwamba yumkini Netanyahu na maafisa kadhaa wa serikali yake wameangamizwa au kujeruhiwa vibaya katika hujuma za makombora ya Iran.
Hivi karibuni, tovuti ya Middle East Minitor iliandika makala ya uchambuzi kuhusu mashambulizi ya kichokozi ya Marekani na utawala wa Kiziayuni wa Israel ikisema kuwa vita hivi ambavyo Benjamin Netanyahu amejiandaa kwa ajili yake kwa miaka mingi yumkini vikapelekea kutengwa kisiasa na kuporomoka stratejia yake.
Kingine kinachobua masuali kuhusu uzima wa Netanyahu ni kufutwa ghafla safari ya Jared Kushner (mkwe wa Rais wa Marekani) na Steve Witkoff, Mjumbe Maalumu wa Donald Trump katika eneo la Asia Magharibi, ambao walitazamiwa kwenda Israel na kukutana na Netanyahu.