Iran yasisitiza Lango la Hormuz halifunguliwi mpaka masharti yake yatimizwe
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140646-iran_yasisitiza_lango_la_hormuz_halifunguliwi_mpaka_masharti_yake_yatimizwe
Mamlaka ya Iran inayosimamia Lango Bahari la Hormuz katika Ghuba ya Uajemi imekanusha vikali madai ya maafisa wa Marekani kuhusu kufunguliwa tena kwa njia hiyo ya kimkakati ya baharini.
(last modified 2026-08-13T10:41:39+00:00 )
Aug 13, 2026 10:39 UTC
  • Lango Bahari la Hormuz
    Lango Bahari la Hormuz

Mamlaka ya Iran inayosimamia Lango Bahari la Hormuz katika Ghuba ya Uajemi imekanusha vikali madai ya maafisa wa Marekani kuhusu kufunguliwa tena kwa njia hiyo ya kimkakati ya baharini.

Mamlaka ya Lango la Ghuba ya Uajemi (PGSA) imeandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X siku ya Jumatano kwamba: “Madai yanayo rudiwa-rudiwa wa maafisa wa Marekani kuwa Lango la Hormuz halijafungwa hayabadili ukweli.”

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa: “Lango la Hormuz bado limefungwa na halitafunguliwa mpaka masharti ya Iran yakubaliwe.”

Iran ilitangaza kufungwa kwa Lango la Hormuz—njia muhimu ya kimataifa ya kusafirishia mafuta—ikiwa ni jibu kwa uchokozi usio na sababu wa Marekani na Israel uliolenga taifa hili.

Vita hivyo vilivyoanza Februari 28 vilimalizika baada ya siku 40 na kisha Marekani na Iran zikatiliana saini mapatnao mwezi o Juni ili kumaliza mzozo uliokuwa umetokana na uchokozi huo.

Jamhuri ya Kiislamu baadaye ilifungua tena lango hilo, lakini ililazimika kulifunga  upya baada ya Marekani kukiuka mapatano na kuingilia utaratibu halali ambao Iran ilikuwa imebuni kusimamia njia hiyo ya kimmkakati.

Mapema mwezi huu wa Agosti, Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa la Iran (SNSC) liliweka sharti la kufunguliwa upya kwa njia hiyo ya maji kutimizwa kwa masharti kama vile Marekani kusitisha kikamilifu uchokozi dhidi ya Iran na washirika wake wa kikanda, kuondolewa kwa kizuizi haramu cha baharini na vikwazo vyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, kurudishwa kwa mali zilizofungiwa za Iran, pamoja na kulipwa fidia kwa uharibifu uliotokana na uchokozi huo.