Jenerali: Jaribio lolote la uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran litasambaratishwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140634-jenerali_jaribio_lolote_la_uvamizi_wa_nchi_kavu_dhidi_ya_iran_litasambaratishwa
Naibu wa Mambo ya Kiutendaji katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utayari wa kijeshi na uwezo wa kimkakati wa jeshi hilo vimelazimisha Marekani kurekebisha malengo yake ya kisiasa mara kwa mara, akionya kuwa jaribio lolote la uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran litasambaratishwa.
(last modified 2026-08-13T04:39:40+00:00 )
Aug 13, 2026 04:37 UTC
  • Iran: Jaribio lolote la uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran litasambaratishwa
    Iran: Jaribio lolote la uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran litasambaratishwa

Naibu wa Mambo ya Kiutendaji katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utayari wa kijeshi na uwezo wa kimkakati wa jeshi hilo vimelazimisha Marekani kurekebisha malengo yake ya kisiasa mara kwa mara, akionya kuwa jaribio lolote la uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran litasambaratishwa.

Brigedia Jenerali Alireza Sheikh alisema siku ya Jumatano kuwa “ustadi wa kimkakati wa Iran katika uwanja wa vita” umeilazimisha Ikulu ya Marekani (White House) kufafanua upya malengo yake ya kisiasa kila mara.

Amekanusha madai ya Marekani kwamba vikosi vya wanamaji vya Iran viliharibiwa kabisa wakati wa uvamizi wa hivi karibuni wa Marekani na utawala wa Kizayuni, akisisitiza kuwa nguvu ya kijeshi haiwezi kupimwa kwa silaha na vifaa pekee.

Brigedia Jenerali Sheikh amesema: “Nguvu si kipengele cha kiufundi kinachoweza kupimwa kwa zana na vifaa pekee. Nguvu ni sanaa ya kupanga mbinu katika uwanja wa vita na kuunganisha uwezo wa ulinzi ili kufikia lengo.”

Amesema nchi inaweza kumiliki teknolojia ya hali ya juu na kupata mafanikio ya kitaktiki katika makabiliano ya moja kwa moja, lakini mafanikio hayo hayamaanishi ushindi wa kimkakati.

Brigedia Jenerali Sheikh amefichua, kuwa utawala wa Kizayuni na Marekani walikuwa wameunda mipango ya kuleta ukosefu wa usalama na kuchochea harakati za kujitenga maeneo magharibi mwa Iran. Amefafanua zaidi kwa kusema kuwa Iran ilijibu kwa kuchukua hatua za mapema kukabiliana na njama hzio. Alipoulizwa kuhusu uwezo wa kuzuia wa makombora ya Iran na uwezo wake wa kujibu vita pana zaidi, Brigedia Jenerali Sheikh amesema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani za Iran bado ziko tayari kwa operesheni.

Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zilianzisha vita vya kichokjozi dhidi ya Iran mnamo Februari 28 kwa kumuua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, pamoja na makamanda waandamizi wa kijeshi, raia wa kawaida wakiwemo watoto.

Hata hivyo, siku 40 baadaye, mnamo Aprili 8, maadui hao walilazimika kukubali usitishaji vita kutokana operesheni za Iran za kulipiza kisasi zilizofanikiwa, na udhibiti madhubuti wa Iran katika Lango la Hormuz.

Iran na Marekani zilitia saini Mkataba wa Maelewano (MoU) wa mnamo Juni 17, lakini Marekani ilivunja makubaliano hayo kwa kuishambulia Iran.

Kama jibu, Vikosi vya Wanajeshi vya Iran vimefanya mashambulizi makali dhidi ya shabaha za kimkakati za Marekani kote katika Asia ya Magharibi.