-
Pezeshkian: Iran kamwe haitasalimu amri mbele ya mashinikizo
Sep 21, 2025 06:52Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu msimamo thabiti wa Iran, na kusema Jamhuri ya Kiislamu itashinda vikwazo vinavyochochewa na wale wote wenye nia mbaya na kamwe haitasalimu amri mbele ya uonevu na matakwa yao ya mabavu.
-
SNSC: Iran kusitisha ushirikiano na IAEA baada ya kuwekewa tena vikwazo
Sep 21, 2025 06:52Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran (SNSC) limesema Tehran itasitisha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kutoiondolea kabisa Tehran vikwazo dhidi yake.
-
Iran yaonya kuwa itasitisha mkataba wa IAEA iwapo vikwazo vya UN vitarejeshwa
Sep 21, 2025 03:25Mwanadiplomasia mwandamizi wa Iran amesema kuwa makubaliano ya hivi karibuni kati ya Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA yaliyofikiwa mjini Cairo yatasitishwa ikiwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa vitarejeshwa au utaratibu unaoitwa snapback.
-
Moscow: Kurejeshwa vikwazo dhidi ya Iran sio halali kisheria
Sep 20, 2025 11:25Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alisema Ijumaa jioni kwamba, kurejeshwa kwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hakuna uhalali wowote wa kisheria na kwamba waliotia saini makubaliano ya nyuklia hawapaswi kuchukua hatua kama hiyo.
-
Iran yalaani jaribio la kichochezi la E3 la kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa
Sep 20, 2025 07:57Iran imelaani vikali jaribio la mataifa matatu ya Ulaya—Uingereza, Ufaransa na Ujerumani—la kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi yake kupitia kile kinachoitwa utaratibu wa “snapback,” na kuitaja hatua hiyo kuwa “kitendo kisicho halali, kisicho na msingi na cha kichochezi”
-
Iran: Baraza la Usalama la UN limeihasiri diplomasia kwa kupinga vikwazo visiondolewe moja kwa moja
Sep 20, 2025 03:41Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, uamuzi wa Baraza la Usalama la umoja huo wa kutoondoa moja kwa moja vikwazo ilivyowekewa Iran unadhoofisha chombo hicho kikuu cha kimataifa, unavuruga diplomasia na unahatarisha Mkataba wa Kuzuia Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Araqchi alitaka Baraza la Usalama la UN kuchagua diplomasia badala ya makabiliano
Sep 20, 2025 02:47Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kuchagua njia ya diplomasia badala ya makabiliano.
-
Sababu za kuongezeka maradufu mauzo ya Iran barani Afrika
Sep 20, 2025 02:33Mauzo ya Iran barani Afrika yameongezeka maradufu.
-
Haj Ali Akbari: Hatutahadaika na mchezo wa Snapback
Sep 19, 2025 13:20Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuhusiana na kuhuishwa utaratibu wa "Snapback" kwamba: Inapasa kuzingatiwa kuwa baada ya kuvuka vikwazo vinavyolemaza; masuala haya kwa kiasi kikubwa ni ya kisaikolojia na ni hila yenye lengo la kupotosha fikra za waliowengi, na kamwe Iran haiwezi kuhadaika na michezo hii.
-
Baghaei: Wafuasi wa utawala katili wa Israel lazima waache kushiriki mauaji ya kimbari
Sep 19, 2025 04:27Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa na kusema kuwa, ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa haikubakisha chembe ya shaka kwamba jinai za Israel huko Ghaza ni mauaji ya kimbari, hivyo waungaji mkono wa utawala huo ghasibu wanapaswa kuacha kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina.