-
Kwa nini Marekani Inahusisha Mgogoro wa Yemen na Iran?
Sep 13, 2026 09:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa madai ya uongo ya Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, hayawezi kubadili uhalisia wa mambo kwamba Ansarallah ya Yemen ni kundi huru linalofanya maamuzi yake lenyewe, halipokei maagizo kutoka kwa mtu yeyote wala kufanya kazi kama kibaraka wa upande mwingine.
-
Rais wa Iran: Tunahitaji mageuzi ya kweli katika mifumo ya kimataifa
Sep 13, 2026 07:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa suala la utawala na mamlaka shirikishi ya dunia na kuimarishwa mfumo wa pande nyingi lina umuhimu mkubwa zaidi hivi sasa.
-
Iran: mkutano wa Oman ni hatua muhimu kuelekea utulivu na usalama wa kikanda
Sep 13, 2026 07:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mkutano uliopangwa kufanyika nchini Oman Jumatatu ya kesho utakuwa hatua muhimu kuelekea kuhakikisha utulivu na usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Iran: Mlango Bahari wa Hormuz unabaki kwenye udhibiti wetu kamili; dunia iilaumu US kwa kupanda bei ya mafuta
Sep 13, 2026 07:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesisitiza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz unasalia kuwa chini ya udhibiti kamili wa Iran, akisema Marekani ndiye wa kulaumiwa kwa kuvurugika usalama wa baharini wa eneo hilo na inapasa ilaumiwe pia kwa kupanda bei ya mafuta duniani.
-
Pezeshkian ahimiza BRICS kuunda mtandao imara wa kibiashara na kutumia sarafu za kitaifa
Sep 12, 2026 04:34Rais Masoud Pezeshkian amezihimiza nchi wanachama wa jumuiya ya BRICS kujenga mtandao thabiti na wenye uwezo wa kustahimili misukosuko ya kibiashara, sambamba na kupanua matumizi ya sarafu za kitaifa ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na mshtuko wa kisiasa.
-
"Falsafa ya Ujumbe wa Mitume ni mwanadamu kusimama imara kupigania haki na uadilifu"
Sep 11, 2026 10:13Imam wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, falsafa ya ujumbe wa Mitume na Manabii ni wanadamu kusimama imara kupigania haki na uadilifu.
-
US yakiri kula kipigo; Iran: Wamarekani msikubali kuwa chambo cha Israel
Sep 11, 2026 09:27Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Wizara ya Vita ya Marekani mapema leo asubuhi amekiri kwamba mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yameangamiza takriban tasisi zote za kijeshi za Marekani nchini Bahrain.
-
Ripoti: Ndege za kivita za Marekani ziliharibiwa katika mashambulizi ya Iran dhidi ya kambi ya kijeshi nchini Jordan
Sep 11, 2026 04:29Ndege kadhaa za kijeshi na kivita za Marekani zinaripotiwa kuharibiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya kambi ya jeshi la anga ya Muwaffaq Salti inayoendeshwa na Marekani, inayojulikana pia kama kambi ya al-Azraq, nchini Jordan.
-
Iran yaiambia IAEA: Ukaguzi wa kawaida wa nyuklia ‘hauwezekani’ katikati ya uchokozi
Sep 10, 2026 10:36Iran imekataa matakwa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwa ajili ya kurejelewa ukaguzi wa kawaida, ikisema kuwa kutarajia utekelezaji wa kawaida wa hatua za usalama huku Iran ikiendelea kukabiliwa na hujuma za kichokozi ni jambo "lisilo na mantiki" na "lisilowezekana kutekelezwa."
-
Wizara ya Ulinzi: Sekta ya ulinzi ya Iran haiwezi kuharibiwa; itastawi na kuimarika pakubwa kuliko huko nyuma
Sep 10, 2026 10:34Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema kuwa sekta ya ulinzi ya nchi hii ni ya ndani, iko imara na imejengwa kwa kutegemea maarifa na uwezo wa vijana wa Iran. Wizara hiyo imesisitiza kuwa sekta hii haiwezi kuharibiwa wala kuangamizwa.