-
"Falsafa ya Ujumbe wa Mitume ni mwanadamu kusimama imara kupigania haki na uadilifu"
Sep 11, 2026 10:13Imam wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, falsafa ya ujumbe wa Mitume na Manabii ni wanadamu kusimama imara kupigania haki na uadilifu.
-
US yakiri kula kipigo; Iran: Wamarekani msikubali kuwa chambo cha Israel
Sep 11, 2026 09:27Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Wizara ya Vita ya Marekani mapema leo asubuhi amekiri kwamba mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yameangamiza takriban tasisi zote za kijeshi za Marekani nchini Bahrain.
-
Ripoti: Ndege za kivita za Marekani ziliharibiwa katika mashambulizi ya Iran dhidi ya kambi ya kijeshi nchini Jordan
Sep 11, 2026 04:29Ndege kadhaa za kijeshi na kivita za Marekani zinaripotiwa kuharibiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya kambi ya jeshi la anga ya Muwaffaq Salti inayoendeshwa na Marekani, inayojulikana pia kama kambi ya al-Azraq, nchini Jordan.
-
Iran yaiambia IAEA: Ukaguzi wa kawaida wa nyuklia ‘hauwezekani’ katikati ya uchokozi
Sep 10, 2026 10:36Iran imekataa matakwa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwa ajili ya kurejelewa ukaguzi wa kawaida, ikisema kuwa kutarajia utekelezaji wa kawaida wa hatua za usalama huku Iran ikiendelea kukabiliwa na hujuma za kichokozi ni jambo "lisilo na mantiki" na "lisilowezekana kutekelezwa."
-
Wizara ya Ulinzi: Sekta ya ulinzi ya Iran haiwezi kuharibiwa; itastawi na kuimarika pakubwa kuliko huko nyuma
Sep 10, 2026 10:34Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema kuwa sekta ya ulinzi ya nchi hii ni ya ndani, iko imara na imejengwa kwa kutegemea maarifa na uwezo wa vijana wa Iran. Wizara hiyo imesisitiza kuwa sekta hii haiwezi kuharibiwa wala kuangamizwa.
-
Kwa nini Ulaya imekuwa tena chombo cha mashinikizo cha Marekani?
Sep 10, 2026 10:16Marekani na kundi la nchi tatu za Ulaya (Troika) zimeungana tena katika mkutano wa Baraza la Magavana la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) katika kushinikiza kupitishwa kwa azimio dhidi ya Iran na kuandaa mazingira ya kupelekwa suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Pakistan: Iran ina haki kisheria ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani
Sep 10, 2026 10:06Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa mwanachama wa Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), ina haki ya kuendeleza mipango yake ya nyuklia kwa malengo ya amani.
-
Vita vya Marekani dhidi ya Iran: Matokeo ya Wazi na ya Siri kwa Wamarekani
Sep 10, 2026 05:40Vita vya Marekani dhidi ya Iran haviwezi kupimwa kwa kuzingatia tu gharama za moja kwa moja za operesheni za kijeshi, ununuzi wa silaha au kuharibiwa vifaa vya kijeshi bali pia vinapaswa kupimwa kutokana na matokeo mengi ya wazi na ya siri kwa wananchi wa Marekani.
-
Msemaji wa Jeshi la SEPAH: Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo Asia Magharibi
Sep 10, 2026 03:22Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo katika eneo la Asia Magharibi.
-
Ripoti: Hatua kali za kulipiza kisasi za Iran zachagiza mipango ya Marekani ya kujiondoa Asia Magharibi
Sep 09, 2026 11:07Maafisa wa jeshi na ujasusi wa Marekani wanajadili kimya kimya kupunguza pakubwa uwepo kijeshi wa Washington katika eneo la Asia Magharibi baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kusababisha vifo vingi na kuharibu kambi na vituo vya ujasusi vya Marekani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya jana Jumanne ya CNN.