Pars Today
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesisitiza kuwa, Iran inaendelea kuunga mkono kwa kila hali harakati za Muqawama au mapambano ya Kiislamu katika eneo.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limewaua au kuwakamata magaidi 69 wanaohusishwa na shirika la ujasusi la Israel, Mossad, wakati wa mazoezi makubwa ya kukabiliana na ugaidi kusini mashariki mwa nchi.
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amevitaja vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza na Lebanon kuwa ni vita kati ya haki na batili.
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba ulimwengu unaelewa kuwa Iran inafuatilia amani na usalama duniani kote na kwamba, mpango wake wa nyuklia ni wa malengo ya amani.
Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Angola na rais wa nchi hiyo wamelaani vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran iko tayari kuketi katika meza ya mazungumzo ya nyuklia na Troika ya Umoja wa Ulaya kulingana na maslahi na haki za Iran na si chini ya mashinikizo na vitisho.
Imesisitizwa katika kikao cha balozi wa Sudan nchini Iran na Mkuu wa kitengo cha matangazo ya nje cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) nia ya dhati ya nchi hizo mbili ya kuendeleza ushirikiano wa vyombo vya habari.
Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA aliwasili mjini Tehran Jumanne jioni ambapo amekutana na kuzungumza na viongozi husika wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, ushirikiano wa Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unaendelea katika fremu ya mkataba wa Kuzuia Utengenezaji na Usambazaji wa Silaha za nyuklia NPT na haki za kimataifa.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameionya Marekani dhidi ya kuanzisha tena kampeni yake ya "mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa" dhidi ya Tehran na kusisitiza kwamba, majaribio ya hapo awali ya Washington ya kuishinikiza Iran yalishindwa na kugonga mwamba.