The Economist: Pipa la mafuta ya petroli litafikia dola 200
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137372-the_economist_pipa_la_mafuta_ya_petroli_litafikia_dola_200
Gazeti la masuala ya kiuchumi la The Economist limeripoti kuwa gharama ya pipa moja la mauta ya petroli itafikia dola 200 iwapo vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vitaendelea.
(last modified 2026-03-15T02:07:26+00:00 )
Mar 15, 2026 02:07 UTC
  • The Economist: Pipa la mafuta ya petroli litafikia dola 200

Gazeti la masuala ya kiuchumi la The Economist limeripoti kuwa gharama ya pipa moja la mauta ya petroli itafikia dola 200 iwapo vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vitaendelea.

Economist limeandika kuwa, baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema iwapo Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa hadi mwishoni mwa mwezi, bei ya mafuta ghafi ya petroli itafikia dola 150 au 200 kwa pipa moja.

Gazeti hilo limesisitiza kuwa jambo hilo litaweka rekodi ya kimataifa.

Kwa sasa pipa moja la mafuta linauzwa kwa dola 140, na ongezeko la dola kumi kwa kila pipa moja la mafuta litayumbisha uchumi wa Marekani.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema, hali ya sasa inashabihiana na ile ya mwaka 2007 kabla ya kuporomoka masoko ya kimataifa.