Seneta wa Marekani afichua uongo wa Trump kuhusu vita dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140074-seneta_wa_marekani_afichua_uongo_wa_trump_kuhusu_vita_dhidi_ya_iran
Seneta Mark Warner wa Marekani amekiri kwamba "hakuna tishio lolote linalokaribia" kutoka kwa Iran dhidi ya Marekani.
(last modified 2026-07-22T06:22:57+00:00 )
Jul 22, 2026 06:20 UTC
  • Seneta wa Marekani afichua uongo wa Trump kuhusu vita dhidi ya Iran

Seneta Mark Warner wa Marekani amekiri kwamba "hakuna tishio lolote linalokaribia" kutoka kwa Iran dhidi ya Marekani.

Mark Warner, seneta wa chama cha Demokrasia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari za Usalama ya Seneti, alisema katika mahojiano ya Julai 19, 2026 na televisheni ya CBS kwamba, akiwa mjumbe wa Kundi la Watu Wanane, ambao ni viongozi wanane wakuu wa bunge walio na uwezo wa kupata habari za kijasusi za kiwango cha juu zaidi, anaweza kusema wazi kwamba hakukuwepo na tishio lolote la karibu dhidi ya Marekani kutoka kwa Iran.

Akibainisha kuwa makombora ya dola milioni 2.5 yanatumiwa kuangusha ndege zisizo na rubani za Iran zenye thamani ya dola 50,000, Warner amekiri kwamba Marekani imeshindwa kabisa kupunguza uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani za Iran.

Akiashiria kwamba vita dhidi ya Iran vilianza "bila mpango," amesema ikiwa mtu atazingatia lengo kuu lililotangazwa rasmi na utawala wa Marekani la kutaka kubadilisha utawala wa Iran, wale walio madarakani kwa sasa nchini Iran ni wabaya zaidi kuliko watangulizi wao.

Seneta Warner amesisitiza kwamba "hakuna maendeleo" yoyote yaliyopatikana katika kufikia madini ya urani iliyorutubishwa ya Iran, jambo linalohitajia wanajeshi 15,000 kuwa katika ardhi ya Iran, lakini hakuna mtu yeyote aliye tayari kufanya hivyo.

Kauli hizi, zilizotolewa na mmoja wa maafisa wenye ujuzi mkubwa wa idara ya ujasusi ya Marekani, zinapingana wazi na madai ya Trump kuhusu sababu za kuanzisha vita na Iran, yaani, "tishio lililokuwa karibu kutokea."

Mnamo tarehe 28 Februari 2020, Rais Donald Trump wa Marekani alianzisha operesheni za kijeshi dhidi ya Iran kwa kisingizio cha "kuondoa tishio lililokuwa linakaribia." Hata hivyo, Warner ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Ujasusi na anayepata taarifa za kijasusi za karibuni kabisa, anasisitiza kwa kusema: "Sikuona taarifa yoyote ya kijasusi iliyoonyesha kuwa Iran ilikuwa karibu kufanya shambulio la kushtukiza dhidi ya Marekani."

Amesisitiza kuhusiana na hili kuwa: "Tishio dhidi ya Marekani halikuwa karibu kutokea. Kwa hivyo, kuweka vikosi na kambi za eneo katika hatari ulikuwa uamuzi binafsi wa Rais, na sio hatua ya kukabiliana na tishio halisi." Jambo la msingi ni kwamba Warner alifanya ukosoaji wa kupinga vita si tu katika miezi ya mwisho ya vita, bali siku chache tu baada ya kuanza vita hivyo, yaani tarehe 1 Machi 2026. Kusisitizwa msimamo huu na afisa mwandamizi wa idara inayopokea taarifa za kijasusi kunaashiria kuwa madai ya "tishio la karibu" yalitiliwa shaka kubwa na jamii inayoshughulikia masuala ya ujasusi ya Marekani.

Suala muhimu ni kwamba, ikiwa "tishio la karibu" ndicho kilikuwa kisingizio cha Trump kuanzisha vita dhidi ya Iran, basi malengo halisi ya vita hivyo yalikuwa yapi? Warner amebainisha kuwa utawala wa Trump ulitumia wiki mbili kamili kufafanua malengo yake, ambayo yalijumuisha kubadilisha utawala, kutwaa urani iliyorutubishwa ya Iran, kudhoofisha uwezo wa Iran wa makombora na ndege zisizo na rubani, pamoja na kulinda usalama wa Lango-Bahari la Hormuz. Hata hivyo, baada ya miezi mitano ya vita visivyo na tija dhidi ya Iran, vilivyosababisha vifo na majeraha mengi kwa wanajeshi wa Marekani, uharibifu mkubwa wa vituo na vifaa vya kijeshi vya Marekani, na gharama zinazofikia takriban dola bilioni 100, hakuna hata lengo moja kati ya hayo lililofikiwa:

Kuhusu suala la mabadiliko ya utawala nchini Iran, Warner amekiri wazi kwa msingi wa fikra za Wamarekani kwamba "wale walio madarakani sasa ni wabaya zaidi kuliko utawala uliopita." Kuhusu urani iliyorutubishwa ya Iran, bado inahifadhiwa katika vituo vilivyo chini ya ardhi; ambapo kuiondoa huko kunahitajia wanajeshi wasiopungua 15,000 wa nchi kavu na kwa muda wa wiki moja.

Kuhusu uwezo wa Iran wa makombora na ndege zisizo na rubani (droni), Warner amesema wazi kuwa, "Tumefeli kabisa kuhusu suala hili." Zaidi ya hayo, tofauti ya gharama katika kukabiliana na makombora na ndege zisizo na rubani za Iran ni ishara ya kufeli kimkakati kwa Marekani. Hatimaye, kuhusu matokeo ya kufungwa Lango-Bahari la Hormuz, Warner amebainisha kuwa bei ya petroli huko Virginia ilikuwa $2.81 kabla ya vita dhidi ya Iran, ambapo sasa imefikia $4.00.

Matamshi ya Mark Warner yanachukuliwa kuwa ya maana sana kwa sababu yeye si mchambuzi wa nje, bali ni mmoja wa maafisa wachache walio na uwezo wa kufikia viwango vyote vya taarifa za kijasusi nchini Marekani, na amedumisha msimamo wake wa kukosoa siasa za Trump tangu mwanzo kabisa wa vita dhidi ya Iran.

Wakati seneta mkuu aliye na hadhi ya kufikia kiwango cha juu zaidi cha habari za kijasusi nchini Marekani anasisitiza mara kwa mara kwamba "hakukuwepo na tishio la karibu," malengo yaliyotajwa ya vita hayajafikiwa na mapendekezo ya wataalamu kuhusu kupunguzwa gharama za vita yanapuuzwa, vita hivi kabla ya jambo lolote, vinakuwa ni vita vya kujitakia na sio vya dharura.

Vita vinavyochochewa kutokana na mambo kutiwa chumvi kupita kiasi kuhusu vitisho au makosa ya tathmini, vita ambavyo vinagharamiwa na roho za askari wa Marekani, kuvurugwa usalama wa Mashariki ya Kati na kodi ya raia wa Marekani. Bila shaka, haya yote yanahudumia maslahi na malengo ya utawala wa Kizayuni, ambao Trump ameahidi kuulinda kwa gharama yoyote ile na kujitolea kikamilifu kutetea maslahi yake bila masharti.