Rais wa Afrika ya Kati afichua sura mpya ya ukoloni
Mar 07, 2026 17:55 UTC
-
Faustin-Archange Touadéra
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema katika: "Diplomasia ya adhabu na vikwazo ni barakoa mpya ya ukoloni."
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra, amesema hayo katika mahojiano yake na RIA Novosti, akifichua sura mpya ya ukoloni.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema katika mahojiano hayo: "Diplomasia ya adhabu na vikwazo ni barakoa mpya ya ukoloni."
Akizungumza na chombo hicho cha habari, Faustin-Archange Touadéra amesema: "Hii leo, ukoloni umebadilisha sura yake. Hii inadhihirishwa, miongoni mwa mambo mengine, kupitia diplomasia ya kulazimisha na hata adhabu, kupitia vikwazo, pamoja na hatua za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja ambazo tunashuhudia kwa sasa."
Tags