Pars Today
Mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano wa Russia na Afrika umeanza leo katika mji wa pwani wa Sochi, kusini mwa Russia; kuashiria muundo mpya wa kawaida wa mazungumzo kufuatia mikutano ya kilele kati ya pande mbili hizo.
Serikali ya Chad imekanusha vikali ripoti kwamba jeshi lake liliwashambulia raia katika operesheni dhidi ya wanamgambo wanaobeba silaha.
Kiongozi mwandamizi wa chama kimoja cha upinzani nchini Cameroon amesema jumuiya ya BRICS ni mbadala halisi wa kuleta mlingano kwenye jiopolitiki duniani na kusisitiza kwamba, nchi za Afrika zinaelewa fika suala hili.
Wataalamu wa mabadiliko ya tabia nchi wametahadharisha kuwa mgogoro wa hali ya hewa Afrika utawaelekeza katika umaskini watu wengine zaidi milioni 150 ifikapo mwaka 2050.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua madhubuti zinapasa kuchukuliwa ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, migogoro na umaskini barani Afrika.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amelitolea wito kundi la BRICS kuwekeza katika maendeleo ya bara la Afrika kwa kuzingatia uwezo wa bara hilo.
Bara la Afrika wiki iliyopita lilisajili vifo vipya 50 vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi wa Mpox na hivyo kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo kufikia 1,100 tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Ripoti hii ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika (Africa CDC).
Mwanaharakati na mwanamajimui mashuhuri wa kupinga ukoloni mamboleo barani Afrika, Stellio Gilles Robert Capo Chichi, maarufu kama Kemi Seba, amekamatwa nchini Ufaransa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa takriban kesi 30,000 zinazoshukiwa kuwa za ugonjwa wa Mpox zimeripotiwa mwaka huu barani Afrika, huku wengi wa walioambukizwa wakitoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa Afrika inapasa kupewa uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC).