Malaysia: Iran inapaswa kupongezwa kwa kusimama kidete dhidi ya mashambulizi ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140742-malaysia_iran_inapaswa_kupongezwa_kwa_kusimama_kidete_dhidi_ya_mashambulizi_ya_marekani
Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim amesema msimamo na azma iliyoonyeshwa na Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani unastahili pongezi.
(last modified 2026-08-17T10:39:08+00:00 )
Aug 17, 2026 10:37 UTC
  • Anwar Ibrahim,Waziri Mkuu wa Malaysia
    Anwar Ibrahim,Waziri Mkuu wa Malaysia

Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim amesema msimamo na azma iliyoonyeshwa na Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani unastahili pongezi.

Anwar amesema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al Jazeera, akibainisha kuwa Malaysia ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimekemea waziwazi mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Waziri Mkuu huyo wa Malaysia ameeleza kwamba, kwa hakika ustahimilivu, kusimama kidete na msimamo thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unastahili pongezi.

Aidha, Anwar Ibrahim ameashiria azimio lililopitishwa na Bunge la Malaysia la kulaani mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, akisema kwamba, Kuala Lumpur imechukua hatua kali zaidi kuliko nchi nyingine nyingi katika kulaani mashambulizi hayo.

Kabla ya hapo, Malaysia ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyolaani vikali mashambulio ya Marekani na utawala vamizi wa Israel dhidi ya Iran, ikisema hatua hiyo inakiuka misingi ya kimataifa.

Malaysia na Iran zina uhusiano wa kidiplomasia na zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali, zikiwemo biashara, uwekezaji, elimu, afya, sayansi na utafiti. Serikali ya Malaysia imesema iko tayari kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.

Uhusiano huo umeendelea kuimarika huku Kuala Lumpur ikichukua msimamo wa kuunga mkono kuheshimiwa kwa mamlaka ya Iran na kulaani mashambulizi dhidi ya Tehran.

Katika mzozo wa sasa, Malaysia pia imechukua msimamo wa kulaani mashambulizi dhidi ya Iran, ikisisitiza kuheshimiwa kwa mamlaka na umoja wa ardhi ya Iran.