Qalibaf: Hatufuatilii kusimamisha vita/kujitanua utawala wa Kizayuni kutasambaratishwa
Mar 10, 2026 10:39 UTC
-
Muhammad Baqir Qalibaf
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa mchokozi anapaswa kumtwangwa ngumi mdomoni ili apate somo na asithubutu kufikiria tena kuivamia Iran.
Muhammad Baqir Qalibaf leo ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akisema: Ni wazi kuwa hatufuatilii suala la kusimamisha vita; tunaamini kuwa tunapasa kumtwanga mgumi mdomoni mvamizi ili asithubutu kufikiria tena kuishambulia nchi yetu pendwa, Iran.
Qalibaf ameongeza kusema: Utawala wa Kizayuni wa Israel unaona uhai wake uliojaa fedheha katika kudumisha mduara wa vita - mazungumzo - usitishaji vita na kuanzisha tena vita kwa madhumuni ya kuimarisha mamlaka na udhibiti wake. Sisi tutakata mduara huu.”