-
Wakuu wa usalama Nigeria waripoti maendeleo katika operesheni ya kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara
Nov 25, 2025 07:29Maafisa wa jeshi la Nigeria wametangaza kuwa kumepigwa hatua nzuri za maenedelea katika jitihada za kukomboa mamia ya wanafunzi wa kike na walimu wao kadhaa waliotekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na silaha katika jimbo la Niger, kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Hemedti atangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja, raia wanaendelea kukimbia makazi yao Sudan
Nov 25, 2025 06:39Kamanda wa waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo “Hemedti”, ametangaza kusitisha mapigano ya ndani kwa kipindi cha miezi mitatu kwa "sababu za kibinadamu", ambako kunajumuisha kusitishwa uhasama; siku moja baada ya mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, kukaataa pendekezo la Marekani kwa ajili ya kusitisha mapigano.
-
IEBC yawataka wanasiasa wa Kenya wasichochee machafuko na uvunjivu wa amani
Nov 25, 2025 06:34Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imewataka wanasiasa kuelekeza nguvu zao katika kuhimiza amani na utulivu, badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea taharuki miongoni mwa wananchi.
-
Familia za watoto waliotekwa nyara Nigeria zachanganyikiwa kutokana na kukaririwa vitendo hivyo mashuleni
Nov 25, 2025 02:43Familia za wanafunzi waliotekwa nyara nchini Nigeria zimenasa kati ya matumaini na kukatishwa tamaa kutokana na vitendo vya kukaririwa vya utekaji nyara wanafunzi wakiwa mashuleni.
-
Mamluki wa kigeni wana jukumu gani katika kuchochea vita nchini Sudan?
Nov 25, 2025 02:39Kamati ya Uchunguzi wa Haki za Binadamu imetangaza kuhusu ushirikiano uliopo kati ya mamluki wa kigeni na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan RSF katika vita vya ndani nchini humo.
-
Al Burhan akataa pendekezo la Marekani, alitaja kuwa baya zaidi kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan
Nov 24, 2025 15:24Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amekataa pendekezo lililowasilishwa na mshauri wa Rais wa Marekani kuhusu masuala ya Kiarabu na Afrika, Massad Boulos, juu ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan.
-
Tanzania kuanza kujenga bandari yenye thamani ya dola bilioni 10 mwezi Desemba
Nov 24, 2025 15:14Tanzania itaanza ujenzi wa bandari mpya mashariki mwa nchi mwezi Desemba mwaka huu na hivyo kumaliza muongo mmoja wa ucheleweshaji kutokana na pingamizi la serikali kwa masharti ya awali ya kandarasi.
-
Raia wengi wakimbia makazi yao baada ya magaidi kuteka nyara mabinti 13 katika jamii ya Borno, Nigeria
Nov 24, 2025 14:39Wimbi la hofu limeikumba jamii ya Borno, na raia wengi wameanza kuondoka majumbani mwao leo Jumatatu, siku mbili baada ya ISWAP, tawi la kundi Boko Haram, kuwateka nyara mabinti 13 wenye umri wa miaka 15 hadi 20.
-
Wanafunzi 50 kati ya 300 waliotekwa Nigeria wafanikiwa kutoroka
Nov 24, 2025 07:11Wanafunzi 50 kati ya 300 waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha kwenye jimbo la katikati mwa Nigeria la Niger, wamefanikiwa kuwatoroka watekaji wao.
-
Guterres: Afrika itagharamika pakubwa licha ya kuchangia kidogo sana mabadiliko ya tabianchi
Nov 24, 2025 03:20Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kuwa Afrika italipa "gharama kubwa" kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi licha ya kuhusika kwake kwa kiwango kidogo sana katika mabadiliko hayo.