Rais wa Nigeria: Wanafunzi wa kike 24 waliotekwa nyara wiki jana wakombolewa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i133616-rais_wa_nigeria_wanafunzi_wa_kike_24_waliotekwa_nyara_wiki_jana_wakombolewa
Wanafunzi wa kike 24 waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule yao ya bweni wiki iliyopita kaskazini magharibi mwa Nigeria wamekombolewa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais.
(last modified 2026-01-01T11:20:11+00:00 )
Nov 26, 2025 07:13 UTC
  • Jeshi la Nigeria
    Jeshi la Nigeria

Wanafunzi wa kike 24 waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule yao ya bweni wiki iliyopita kaskazini magharibi mwa Nigeria wamekombolewa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais.

"Rais Bola Tinubu amekaribisha kuachiliwa huru jana wanafunzi hao wa kike 24  waliotekwa nyara na magaidi huko Maga, katika jimbo la Kebbi, tarehe 17 mwezi huu wa Novemba," imeeleza taarifa iliyosomwa na Bayo Onanuga, Mshauri Maalumu wa Rais wa Nigeria.

Mamlaha husika nchini Nigeria zimearifu kuwa  genge la watu kadhaa lililokuwa limejihami kwa silaha za kisasa huku wakifyatua risasi lilishambulia shule hiyo ya bweni usiku kucha na kumuuwa afisa wa shule hiyo na kumjeruhi mlinzi mmoja.  

Baada ya hujuma hiyo, genge hilo la watu wenye silaha liliwateka nyara mabinti 24 hata hivyo mmoja alifanikiwa kulitoroka genge hilo la wahalifu. 

Rais wa Nigeria amezipongeza idara za usalama na kuzitaka kuzidisha juhudi ili kuwakomboa wanafunzi waliobaki mikononi mwa watekaji nyara.

Watoto zzaidi ya 300 wametekwa nyara katika shule ya Kikatoliki katika jimbo la kati-magharibi mwa Nigeria huku waumini 38 wakitekwa nyara katika kanisa moja mashariki mwa nchi hiyo.