-
Rais wa Nigeria: Wanafunzi wa kike 24 waliotekwa nyara wiki jana wakombolewa
Nov 26, 2025 07:13Wanafunzi wa kike 24 waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule yao ya bweni wiki iliyopita kaskazini magharibi mwa Nigeria wamekombolewa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais.
-
Raia wengi wakimbia makazi yao baada ya magaidi kuteka nyara mabinti 13 katika jamii ya Borno, Nigeria
Nov 24, 2025 14:39Wimbi la hofu limeikumba jamii ya Borno, na raia wengi wameanza kuondoka majumbani mwao leo Jumatatu, siku mbili baada ya ISWAP, tawi la kundi Boko Haram, kuwateka nyara mabinti 13 wenye umri wa miaka 15 hadi 20.
-
Wanafunzi 303, walimu 12 watekwa nyara na watu wenye silaha katika skuli ya jimbo la Niger, Nigeria
Nov 23, 2025 06:33Jumuiya ya Wakristo ya Nigeria (CAN) imetangaza kuwa, jumla ya wanafunzi 303 na walimu 12 wametekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana likiwa ni tukio la pili kubwa kutokea ndani ya wiki moja, huku hofu za usalama zikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
-
Mahakama ya Nigeria yamhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa Wabiafra wanaopigania kujitenga
Nov 22, 2025 02:41Mahakama ya Nigeria imemhukumu Nnamdi Kanu, kiongozi wa harakati ya kupigania kujitenga ya Watu wa Asili wa Biafra (IPOB), kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na hatia ya mashtaka yote saba aliyoshtakiwa yanayohusiana na ugaidi.
-
Nigeria yafunga shule katika jimbo la Kwara kufuatia ongezeko la ukosefu wa usalama
Nov 21, 2025 03:01Mamlaka husika katika Jimbo la Kwara nchini Nigeria zimefunga shule zote katika eneo la Iflodun, Ekiti, Irepodun, Isin na Oke Ero kufuatia vitisho vipya vya usalama katika jimbo hilo.
-
Rais wa Nigeria athibitisha kuuawa afisa wa ngazi ya juu wa jeshi
Nov 19, 2025 12:24Rais wa Nigeria amethibitisha kuwa Brigedia jenerali Musa Uba ameuawa na kundi la kigaidi akiwa matekani. Mauaji hayo yamefanywa siku chache baada ya afisa huyo wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la ISWAP kufuatia shambulio la kuvizia kaskazini mashariki mwa Jimbo la Borno ambalo pia liliwaua wanajeshi wanne.
-
Mkuu wa jeshi la Nigeria aagiza kutafutwa usiku na mchana mabinti wa shule waliotekwa nyara
Nov 19, 2025 02:23Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria ameviagiza vikosi vya jeshi hilo kuendesha msako wa "usiku na mchana" ili kuwanusuru mabinti 25 wa shule waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
-
Magaidi 200 wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi nchini Nigeria
Nov 11, 2025 02:56Mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya magaidi wasiopungua 200 katika eneo la Ziwa Chad.
-
Waislamu na Wakristo wa Nigeria wapinga vitisho vya Trump
Nov 05, 2025 03:11Waislamu na Wakristo wa Nigeria wamesisitiza kuishi pamoja kwa amani na maelewano na kusema kuwa vitisho vya Rais wa Marekani dhidi ya nchi hiyo havikubaliki.
-
Nigeria yapinga vikali vitisho vya Trump, yasema mamlaka yake ya kujitawala hayajadiliwi
Nov 02, 2025 10:41Serikali ya Nigeria imepinga vikali uingiliaji wowote wa kigeni katika mambo ya ndani ya nchi hiyo ikisisitiza kwamba "mamlaka ya kitaifa hayawezi kujadiliwa," na kwamba inachunguza matukio ya hivi karibuni na kuwafuatilia wale wote waliohusika.