-
Amnesty yaikosoa Nigeria kwa kuwakandamiza Waislamu wakiitetea Gaza
Aug 21, 2025 05:13Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International nchini Nigeria, Isa Sunusi, amelaani vikali ukandamizaji mkali wa vyombo vya serikali dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, wakati wa maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kusema kuwa takriban wanachama 83 wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria bado wako rumande bila kufunguliwa mashtaka, licha ya kupata majeraha ya risasi na makovu mengineo wakishiriki maandamano ya amani.
-
Watu 27 wauawa katika shambulio la kigaidi msikitini Nigeria
Aug 20, 2025 06:46Magaidi waliokuwa na silaha jana Jumanne waliwauwa waumini karibu 27 waliokuwa msikitini katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Zakzaky: Mipango ya kuwafukuza Wapalestina Gaza, kuipokonya silaha Hizbullah itafeli
Aug 19, 2025 10:44Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Yaqoub Zakzaky amebainisha kuwa, mipango ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza katika ardhi yao na kuipokonya silaha Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwa kutumia serikali ya Beirut itagonga mwamba.
-
Wanahabari Nigeria walaani mauaji ya waandishi wenzao huko Gaza
Aug 18, 2025 06:43Muungano wa Waandishi wa Habari wa Nigeria (NUJ) umelaani vikali mauaji ya wanahabari yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa, hujuma hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wenzao katu haziwezi kuwazuia wahudumu wa tasnia hiyo kuendelea kufichua ukweli.
-
Operesheni ya pamoja ya AUSSOM na jeshi la Somalia yaangamiza zaidi ya magaidi 50 wa Al Shabab
Aug 04, 2025 11:02Vikosi vya Umoja wa Afrika vya Usaidizi na Kuleta Uthabiti nchini Somalia vimetangaza kuwa, zaidi ya magaidi 50 wa kundi la Al Shabab wameuawa katika operesheni ya pamoja iliyotekelezwa na vikosi hivyo na jeshi la Somalia (SNAF) katika mji wa Bariire, huko Lower Shabelle.
-
Kufuatia hatua ya TZ, EAC yazitolea mwito nchi wanachama ziheshimu mpango wa soko la pamoja
Aug 01, 2025 07:17Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Nduva, amezitaka nchi wanachama za jumuiya hiyo kutekeleza mikataba yenye kuheshimu mpango wa soko la pamoja kwa ajili ya kufikia utangamano wa kikanda.
-
Mlipuko wa kipindupindu wauwa watu 13 katika jimbo la Niger, nchini Nigeria
Jul 24, 2025 10:31Takriban watu 13 wamefariki dunia na wengine 239 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kuenea katika wilaya sita za jimbo la Niger katikati mwa Nigeria. Taarifa hii imetolewa na mamlaka husika katika jimbo la Niger.
-
Maisha ya watu milioni 1.3 Nigeria yako hatarini baada ya WFP kusitisha misaada
Jul 24, 2025 06:49Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa litalazimika kusitisha msaada wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 katika eneo lililokumbwa na machafuko zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa mwezi huu wa Julai kutokana na hifadhi yake ya chakula na virutubisho vya lieshe kumalizika.
-
6 wauawa, 100 watekwa katika shambulio la majambazi Zamfara, Nigeria
Jul 18, 2025 16:35Watu wenye silaha wameripotiwa kuwauwa watu wasiopungua sita na kuwateka nyara wengine zaidi ya 100, wakiwemo wanawake na watoto, katika shambulio dhidi ya watu wa jamii ya Kairu katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Novak: Ushirikiano wa Russia, Nigeria ni muhimu kwa uthabiti wa soko la mafuta
Jul 16, 2025 13:33Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Alexander Novak amesema ushirikiano wa nchi hiyo na Nigeria katika fremu ya OPEC+ una nafasi muhimu katika kudumisha uthabiti wa soko la mafuta duniani.