-
Polisi wa Nigeria wawakomboa mateka baada ya makabiliano ya risasi na watekaji nyara
Jan 06, 2025 13:20Polisi ya Nigeria imeripoti kuwa mateka wanne waliotekwa nyara wamekombolewa baada ya makabiliano ya risasi na watekaji nyara katika jimbo la Imo kusini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Rais wa Nigeria apongeza mpango wa nchi hiyo wa mabadiliko ya kodi
Dec 25, 2024 02:18Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema kuwa atasonga mbele na miswada minne ya marekebisho ya kodi ambayo tayari imewasilishwa bungeni licha ya kukabiliwa na radiamali hasi ya magavana kadhaa wa majimbo nchini humo.
-
Watu zaidi ya 20 wapoteza maisha katika mkanyagano wakati wa ugawaji wa chakula huko Nigeria
Dec 21, 2024 14:01Takriban watu 20 wamepoteza maisha katika tukio la mkanyagano lililotokea katika zoezi la ugawaji chakula katika Jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria.
-
Watoto 32 waaga dunia katika mkanyagano kwenye tamasha la wanafunzi nchini Nigeria
Dec 19, 2024 11:21Kamanda wa Polisi katika jimbo la Oyo nchini Nigeria, Adewale Osifeso, amesema kuwa watoto wasiopungua 32 wamethibitishwa kufariki dunia katika mkanyagano wa jana kwenye tamasha la wanafunzi jimboni humo.
-
Magenge yenye silaha yauwa watu 30 katika muda wa siku 3 huko Benue, Nigeria
Nov 26, 2024 02:54Watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya magenge yenye silaha yaliyojiri kwa muda wa siku tatu dhidi ya wakulima jamii mbalimbali katika jimbo la Benue kaskazini kati nchini Nigeria.
-
Wanajeshi wasiopungua 12 wa Nigeria wauawa katika hujuma ya Boko Haram
Nov 20, 2024 12:07Wanajeshi zaidi ya 12 wa Nigeria waliuliwa jana Jumanne katika mashambulizi kadhaa ya kundi la kigaidi la Boko Haram dhidi ya kambi ya jeshi katika jimbo la Borno kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Jeshi la Nigeria laua 'magaidi' 187 ndani ya wiki moja
Nov 03, 2024 06:16Zaidi ya watu 187 wanaoshukiwa kuwa magaidi wameuawa huku wengine 262 wakikamatwa katika operesheni mbalimbali za kupambana na ugaidi za jeshi la Nigeria nchini kote katika muda wa wiki moja iliyopita.
-
Wabeba silaha waua wanakijiji 15 katika jimbo la Benue, Nigeria
Nov 01, 2024 09:39Kwa akali watu 15 wameuawa katika shambulizi la 'majambazi' waliojizatiti kwa silaha katika jimbo la Benue katikati mwa Nigeria.
-
Wahanga wa mlipuko wa lori la mafuta Nigeria wazikwa kwa umati
Oct 17, 2024 07:58Maafisa wa serikali za mitaa kaskazini mwa Nigeria jana waliungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya maziko ya umati ya zaidi ya wahanga 140 waliopoteza maisha katika mlipuko mkubwa wa lori la mafuta usiku wa kuamkia jana.
-
Watu 21 wafariki dunia baada ya boti kugongana nchini Nigeria
Oct 09, 2024 07:03Polisi ya Nigeria jana ilithibitisha kupoteza maisha takriban watu 21 baada ya boti mbili za abiria ambazo hazikuwa zimesajiliwa kupinduka. Boti hizo zilipinduka baada ya kugongana katika jimbo la Lagos nchini Nigeria.