Mwanachuoni Nigeria: Israel itafutwa katika uso wa dunia ikiishambulia tena Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135238-mwanachuoni_nigeria_israel_itafutwa_katika_uso_wa_dunia_ikiishambulia_tena_iran
Mwanachuoni mashuhuri wa Kiislamu wa kaskazini mashariki mwa Nigeria amezionya Israel na Marekani dhidi ya kufanya mashambulizi yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran, akisema matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi kuliko yale ya vita vya siku 12 vya mwezi Juni mwaka uliopita 2025, na kuilazimisha Israel kuomba usitishaji vita.
(last modified 2026-01-08T06:08:54+00:00 )
Jan 08, 2026 06:08 UTC
  • Mwanachuoni Nigeria: Israel itafutwa katika uso wa dunia ikiishambulia tena Iran

Mwanachuoni mashuhuri wa Kiislamu wa kaskazini mashariki mwa Nigeria amezionya Israel na Marekani dhidi ya kufanya mashambulizi yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran, akisema matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi kuliko yale ya vita vya siku 12 vya mwezi Juni mwaka uliopita 2025, na kuilazimisha Israel kuomba usitishaji vita.

Sheikh Ahmad Yusuf Yashi ameeleza bayana kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimsingi ni tofauti na nchi nyingine zilizowahi kulengwa na kushambuliwa na Washington huko nyuma.

Amebainisha kuwa, "Marekani na utawala wa Kizayuni zinaweza kuhadaika na vitendo vyao vya huko nyuma mahali pengine, lakini zinapaswa kuelewa kwamba, ikiwa watakariri yale waliyofanya mwezi Juni (2025), Israel inaweza kufutwa kabisa katika uso wa dunia." 

Msomi huyo mashuhuri wa Kiislamu nchini Nigeria amesisitiza kuwa, jibu la Iran kwa uchokozi wowote mpya litakuwa la nguvu, maangamivu na lisilotabirika.

Kadhalika Sheikh Ahmad Yusuf amesema vita vya Siku 12 ilivyotwishwa Iran viliimarisha umoja wa ummah wa Kiislamu, na kuongeza kuwa hata Wakristo duniani kote waliungana kuiunga mkono Iran.

"Marekani na utawala wa Kizayuni wanaweza kughilibiwa na vitendo vyao vya zamani mahali pengine, lakini wanapaswa kuelewa kwamba ikiwa watarudia yale waliyofanya mwezi Juni, Israel inaweza kufutwa kabisa," ameonya mwanachuoni huyo wa Nigeria.

Kiongozi huyo mashuhuri wa kidini nchini Nigeria amesisitiza kuwa, jibu la Iran kwa uchokozi wowote mpya litakuwa zito na kubwa.