Nigeria yauwa magaidi 40 wa Boko Haram katika operesheni za anga
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135666-nigeria_yauwa_magaidi_40_wa_boko_haram_katika_operesheni_za_anga
Jeshi la Anga la Nigeria limetangaza kuwua limeuwa takriban magaidi 40 wa Boko Haram katika mashambulizi ya anga mtawalia iliyofanya mapema wiki hii katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
(last modified 2026-01-19T11:34:11+00:00 )
Jan 19, 2026 11:34 UTC
  • Jeshi la anga la Nigeria
    Jeshi la anga la Nigeria

Jeshi la Anga la Nigeria limetangaza kuwua limeuwa takriban magaidi 40 wa Boko Haram katika mashambulizi ya anga mtawalia iliyofanya mapema wiki hii katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa Jeshi la Anga la Nigeria Ehimen Ejodame amesema kuwa oparesheni hizo zilifanywa Alhamisi na Ijumaa kwa kulenga maficho ya magaidi wa boko Haram na kupelekea kuuliwa wanachama kadhaa wa kundi hilo.

Nigeria imekuwa katika mapambano ya muda mrefu dhidi ya Boko Haram na vijikundi vilivyogawanyika vyenye mfungamano na kundi hilo tangu mwaka 2009. Hujuma za Boko Haram zimegharimu makumi ya maelfu ya maisha na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao katika Bonde la Ziwa Chad, na kuathiri nchi jirani kama vile Cameroon, Chad na Niger.

Mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya  Nigeria yanawakilisha juhudi zinazoendelea za Jeshi la Anga la nchi hiyo wa kudhoofisha uwezo wa kiutendaji wa vikundi vay wahalifu wenye silajha katika eneo hilo, hasa katika ngome zao ndani ya jimbo la Borno.

Hii ni katika hali ambayo, pamoja na kufanikiwa jeshi la Nigeria katika kupambana na magaidi wenye silajha, lakini hujuma wanazoendelea kufanya ni tishio kuu kwa usalama. 

Ukosefu wa usalama mara nyingi umekuwa ukivuruga shughuli za kilimo, biashara na usambazaji wa misaada ya kibinadamu na kuzidisha uhaba wa chakula kwa wananchi. 

Serikali ya Nigeria inasisitiza kuwa operesheni kama hizo za kijeshi ni muhimu ili kutayarisha mazingira ya kurejea salama kwa watu waliokimbia makazi yao na kurejesha mamlaka za serikali katika maeneo yaliyoathirika.