Trump: Marekani ‘itajihusisha kwa nguvu’ katika sekta ya mafuta ya Venezuela
-
Sekta ya mafuta ya Venezuela na ushiriki wa Marekani
Katika matamshi yake ya uingiliaji kati, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa Washington itakuwa na nafasi kuu katika sekta ya mafuta ya Venezuela kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya jana ya Marekani dhidi ya Caeacas yaliyopelekea kukamatwa Rais wa Venezuela Nicolas maduro.
Akizungumza jana na televisheni ya Fox News, Trump amejigamba kuwa: Marekani itashiriki pakubwa katika sekta ya mafuta ya Venezuela. Amesema Marekani ina makampuni makubwa ya mafuta duniani na kwamba Washington itahusika pakubwa katika sekta ya mafuta ya Venezuela.
Rais Donald Trump wa Marekani amethibitisha kuwa nchi yake imemkamata mwenzake wa Venezuela Nicolas Maduro.
Marekani imeeleza haya baada ya kuripotiwa mashambulio mazito katika mji mkuu wa Venezuela mapema jana Jumamosi.
"Marekani imefanikiwa kutekeleza shambulio kubwa dhidi ya Venezuela na kiongozi wake, Rais Nicolas Maduro, na mke wake wamekamatwa na kuondolewa nchini mwao” Rais Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.
Wakati huo huo JD Vance Makamu wa Rais wa Marekani amedai kuwa Rais wa Venezuela alipatiwa fursa nyingi kabla ya yeye na mkewe kukamatwa na jeshi la Marekani.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Nishati yenye makao yakek mjini London Uingereza, Venezuela ina akiba kubwa ya mafuta duniani. Venezuela ina akiba ya mapipa ya mafuta yasiyopungua bilioni 303 au asilimia 17ya akiba yote ya dunia na hivyo kuipita Saudi Arabia.
Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela yamejiri kufuatia mashinikizo ya miezi kadhaa ya Wahsington dhidi ya Caracas kwa kisingizio cha eti kupambana na magendo ya mihadarati.
Serikali ya Caracas kwa upande wake imekanusha mara kadhaa madai ya Marekani na kusema haihusiki kivyovyote katika magendo ya madawa ya kulevya na kusisitiza kuwa Washington ina lengo la kumpindua Rais wa Venezuela lengo likiwa ni kudhibiti visima vikuvya vya mafuta vya nchi hiyo.