Venezuela, mwathirika mpya wa sera inayojikariri ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135074-venezuela_mwathirika_mpya_wa_sera_inayojikariri_ya_marekani
Tangazo la Rais Nicolás Maduro la kuwa tayari kufanya mazungumzo na Marekani limejibiwa chini ya saa 24 baadaye kwa mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya Caracas, huu ukiwa ni mtindo unaokaririwa wa viongozi wa Washington.
(last modified 2026-01-03T16:08:36+00:00 )
Jan 03, 2026 13:24 UTC
  • Venezuela, mwathirika mpya wa sera inayojikariri ya Marekani

Tangazo la Rais Nicolás Maduro la kuwa tayari kufanya mazungumzo na Marekani limejibiwa chini ya saa 24 baadaye kwa mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya Caracas, huu ukiwa ni mtindo unaokaririwa wa viongozi wa Washington.

Mji mkuu wa Venezuela, Caracas, imelipuliwa kwa bomu mapema alfajiri ya leo, chini ya saa 24 baada ya Rais wa nchi hiyo, Nicolás Maduro, kutangaza kwamba visima vyake vya mafuta viko wazi kwa Wamarekani na kutoa wito wa mazungumzo na serikali ya Washington. Alkhamisi usiku, vyombo vingi vya habari vya dunia vilisambaza ujumbe wa video wa Maduro akisema yuko tayari kuingia kwenye mazungumzo na Marekani.

Katika mahojiano na televisheni ya taifa ya Venezuela, Maduro alisema yuko tayari kuzungumza na Marekani "wakati wowote na mahali popote wanapotaka." Hata hivyo msimamo huo laini wa Maduro haukuweza kuwashawishi Wamarekani kuingia kwenye mazungumzo, bali chini ya saa 24 baada ya tangazo hilo, Marekani imeishambulia Caracas kwa mabomu na kumpeleka  Nicolás Maduro kusikojulikana. 

Inaonekana hakuna mabadiliko katika sera na mienendo hii ya kijuba ya Marekani. Yeyote anayetaka kufanya mazungumzo na Marekani hujibiwa kwa ngumi ya chuma na kupigwa mabomu. Katika miongo miwili iliyopita, Marekani imekariri kufanya uvamizi wa kijeshi au mashambulizii ya mabomu baada ya upande mwingine kupunguza makali na kukubali kufanya mazungumzo na hata kushambuliwa katikati ya mazungumzo. Ili kuweka wazi zaidi uikweli huu tunaashiria mifano kadhaa:

Kwanza ni Afghanistan, 2001. Baada ya mashambulizi ya Septemba 11, Marekani ilifanya mazungumzo ya siri na baadhi ya makundi na nchi kadhaa katika kanda hiyo ya Asia ili kushirikiana katika mapambano dhidi ya al-Qaeda, lakini wakati huo huo, ilianzisha mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya kambi za Taliban na al-Qaeda.

Pili ni Iraq hapo mwaka 2003. Wakati mazungumzo ya kidiplomasia yalipokuwa yakiendelea baina ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa nchi hiyo ili kukagua silaha za Iraq na kutatua mvutano uliokuwapo na Saddam Hussein, Marekani ilianzisha mashambulizi ya kijeshi na kusababisha vita vya Iraq vilivyoua maelfu ya raia wasio na hatia.

Huko Syria, 2018 Marekani na washirika wake walianzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo kabla ya kuanza mazungumzo rasmi kuhusu kadhia ya kupunguza mvutano, licha ya kwamba Umoja wa Mataifa na pande zingine zilikuwa ziikifanya upatanishi.

Mwezi Juni mwaka uliomalizika majuzi, Marekani na Israel zilishambulia vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia vya Iran wakati ambapo mazungumzo ya nyuklia kati ya Tehran na Washington yalikuwa yamemaliza raundi tano, na pande hizo zilikijitayariisha kwa mazungumzo ya raundi ya sita.

Mapema leo, katika siku za mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2026, Marekani imekariri ushetani wake kwa kuushambulia mji wa Caracas ili kuhakikisha kwamba sera yake ya kutumia mabavu katika mahusiano ya kimataifa, inaendelea!

Uzoefu na tajiri hii inaonyesha kwamba kufanya mazungumzo na Marekani hakuna faida yoyote, bali kinyume chake, kuna madhara makubwa kwa nchi zinazolengwa. Tunapopitia kwa haraka mifano ya kihistoria tunaona kwamba neno "mazungumzo" kwa Marekani ni sawa kabisa na "kuwa tayari kwa ajili ya kushambuliwa."

Mchakato huu ni somo la kihistoria kwa ulimwengu mzima kwamba: kuingia kwenye mazungumzo na Marekani kuna maana ya kukubali kibubusa matakwa yote ya serikali ya Washington. Kwa msingi huo walimwengu hawana isipokuwa machaguo mawili tu kwa ajili ya kukabiliana na dhulma na uonevu wa Marekani: Ama kujisalimisha kabisa au muqawama na mapambano!