Hamas yailaani vikali Israel kwa kuendelea kukiuka usitishaji vita Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135132-hamas_yailaani_vikali_israel_kwa_kuendelea_kukiuka_usitishaji_vita_gaza
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeilaani vikali Israel kwa kuendelea kukiuka makubaliano ya usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa hatua kama hizo zinatishia kudhoofisha makubaliano hayo yanayolegalega.
(last modified 2026-01-05T07:58:41+00:00 )
Jan 05, 2026 07:58 UTC
  • Hazem Qassem
    Hazem Qassem

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeilaani vikali Israel kwa kuendelea kukiuka makubaliano ya usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa hatua kama hizo zinatishia kudhoofisha makubaliano hayo yanayolegalega.

Hazem Qassem, msemaji wa Hamas amewatuhumu askari jeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kuwalenga na kuwauwa shahidi raia na kuvuka mistari iliyoainishwa katika maeneo kama Khan Yunis; jambo linalowalazimisha Wapalestina kuhama makazi yao. 

Msemaji wa Hamas ameashiria ongezeko kubwa la ubomoaji nyumba mashariki kwa Gaza na kuzitaja hatua hizo kuwa sehemu ya mauaji ya kimbari na maangamzi ya kizazi yanayofanywa na Israel katika maeneo ya mijini. 

Hazem Qassem amewatolea wito wapatanishi na nchi zilizosimamia makubaliano ya kusitisha vita kuzidisha mashinikizo kwa Israel na kuulazimisha utawala huo uache kukiuka makubaliano hayo na utekelezea wajibu wake kwa mujibu wa makubaliano hayo. 

Israel imekiuka makubaliano ya kusimamisha vita kwa mara mia kadhaa tangu kuanza utekelezaji wake, ikiwemo kufanya hujuma kubwa na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza. 

Aidha Wapalestina wawasiopungua 420 wameuawa shahidi na 1,200 kujeruhiwa tangu kuanza kutekelezwa makubalio ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya Israel na Hamas.