Pars Today
Kundi la magaidi wakufurishaji limeyafyatulia risasi magari ya abiria yaliyokuwa yamebeba raia Waislamu wa madhehebu ya Shia kaskazini-magharibi mwa Pakistan na kuua karibu watu 40 na kujeruhi wengine 30 katika moja ya mashambulizi mabaya zaidi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni kwenye eneo hilo lenye machafuko.
Hamjambo na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi chetu cha leo ambacho kinaendelea kuzungumzia sababu za kuendelea kusimama imara kambi ya Muqawama dhidi ya mabeberu na utawala wa Kizayuni wa Israel...
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amepuuzilia mbali ripoti za baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kufungwa kwa ofisi ya Harakati ya Muqawamawa wa Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Doha.
Kamanda wa Kikosi cha 401 cha jeshi la Israel ameuawa na wanamuqawama wa Palestina kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, jeshi la Israel limethibitisha.
Wanajeshi kadhaa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na kujeruhiwa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kati la Ukanda wa Ghaza na kusababisha moto mkubwa uliopelekea kuuawa shahidi Wapalestina waliokuwa wametafuta hifadhi kwenye eneo hilo kutokana na hilaki ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala huo ghasibu.
Mjumbe mmoja wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameshukuru matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika khutba ya Sala ya Ijumaa kwa kutaja oparesheni za makombora za Iran dhidi ya utawala huo katili wa Kizayuni kuwa ni za kihistoria.
Assalamu Alaykum wapenzi wasikilizaji. Karibuni kuwa nami katika kipindi hiki maalumu tulichokuandalieni kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza habari ya kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut, Hamas imeonya kuwa, hatua hizo hazitaifanya Israel kuwa sehemu salama zaidi.