-
Russia na Msumbiji zathibitisha tena ushirikiano wa kiulinzi baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje
Jul 23, 2025 10:56Russia na Msumbiji zimetihibitisha kwa mara nyingine ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi mbili hizo kufuatia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji mjini Moscow.
-
Ufaransa yasisitiza uwakilishi zaidi wa nchi za Kiafrika katika Baraza la Usalama la UN
Jul 23, 2025 10:51Mwakilishi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Paris inaunga mkono kufanyika mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) ili kuongeza uwakilishi wa mataifa ya Afrika katika taasisi hiyo ya kimataifa.
-
Katika wiki moja vifo 18, maambukizi 1,300 ya kipindupindu yaripotiwa Sudan iliyogubikwa na vita
Jul 23, 2025 06:12Wizara ya Afya ya Sudan imeripoti maambukizi mapya ya kipindupindu, huku idadi hiyo ikifika 1,307 na vifo 18 vilivyosababishwa na ugonjwa huo ndani ya muda wa wiki moja.
-
Raila Odinga: Sikufaidika na hendisheki ya Uhuru Kenyatta
Jul 23, 2025 03:41Kiongozi wa chama cha ODM nchini Kenya, Bwana Raila Odinga amepuuza madai yanayosema kuwa alinufaika kutokana na ushirikiano kati yake na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyatta, akisema hakupewa nafasi yoyote serikalini au kupata manufaa ya kibinafsi.
-
Wagombea 81 wachukua fomu ya kuwania kiti cha urais Cameroon
Jul 22, 2025 14:09Jumla ya wagombea 81 wamejaza fomu na kuwasilisha kwa Tume ta Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi wa Rais wa Oktoba mwaka huu.
-
Jeshi Mali lamuangamiza kinara wa Daesh katika eneo la Sahara
Jul 22, 2025 04:37Jeshi la Mali limetangaza kuwa limemuua Souleymane Ag Bakawa, mmoja wa viongozi wa kundi la kigaidi la Daesh katika eneo pana la Sahara, wakati wa operesheni ya kiusalama katika eneo la Tinfadimata, kaskazini mwa Mali.
-
Al-Burhan: Tuna uwezo wa kuwashinda waasi wa RSF, tunapinga uingiliaji wa kigeni
Jul 22, 2025 04:33Mkuu wa Baraza la Ukuu wa Uongozi wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan amesema vikosi vya jeshi la Sudan vina uwezo wa kushinda kile alichokiita "wanamgambo wa Dagalo," akimaanisha Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo.
-
Mwanaharakati wa haki za binadamu Kenya aachiwa kwa dhamana, ashtakiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria
Jul 21, 2025 13:38Boniface Mwangi, mwanaharakati wa haki za binadamu wa Kenya ambaye amekuwa na nafasi kuu katika maandamano dhidi ya serikali, ameachiwa huru kwa dhamana leo Jumatatu baada ya kushtakiwa kwa kupatikana na gesi ya kutoa machozi na silaha nyumbani kwake.
-
Rais wa Eritrea aitahadharisha Ethiopia juu ya kuibuka mzozo mpya
Jul 21, 2025 13:29Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki, ametoa tahadhari kwa jirani yake Ethiopia, na kuonya juu ya uwezekano wa kuzuka mzozo mpya kati ya nchi mbili huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika eneo la Pembe ya Afrika.
-
Magaidi 70 waangamizwa katika operesheni za jeshi nchini Mali
Jul 20, 2025 16:23Jeshi la Mali lilitangaza jana Jumapili kwamba, magaidi wasiopungua 70 waliuawa katika operesheni mbili za kiusalama kaskazini na katikati mwa nchi.