Israel yafanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135178-israel_yafanya_mashambulizi_makubwa_ya_anga_dhidi_ya_lebanon
Israel imefanya mfululizo wa mashambulizi ya anga katika maeneo yote ya kusini na mashariki mwa Lebanon, ikiendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo lengo lake ni kukomesha uchokozi wa Israeli dhidi ya uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2026-01-06T12:10:08+00:00 )
Jan 06, 2026 12:10 UTC
  • Israel yafanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Lebanon

Israel imefanya mfululizo wa mashambulizi ya anga katika maeneo yote ya kusini na mashariki mwa Lebanon, ikiendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo lengo lake ni kukomesha uchokozi wa Israeli dhidi ya uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu.

Mashambulizi hayo yaliyofanyika kwenye miji ya al-Manara katika eneo la Bekaa na wilaya ya Jezzine kusini mwa Lebanon yalifuatia vitisho vilivyotolewa na Israel na kupelekea familia nyingi kuondoka kwenye maeneo hayo.

Wakati huo huo televisheni ya Al Jazeera imemnukuu afisa mmoja wa Hamas akisema kwamba, utawala wa Kizayuni huwa unabuni visingizio vya uongo ili kuhalalisha mashambulizi yake dhidi ya watu wa Palestina huko Ghaza na Lebanon. Afisa huyo wa HAMAS ameongeza kuwa, madai ya Israel kuhusu kuweko silaha za harakati hiyo kuwa Lebanon hayana msingi na yanatumika kama kisingizio tu cha kuhalalisha mashambulizi dhidi ya wakimbizi wa Palestina walioko Lebanon.

Taarifa zinasema kuwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Palestina kwa kifupi UNRWA ndilo lenye kambi kubwa zaidi kati ya kambi 12 za wakimbizi wa Palestina nchini Lebanon na ina watu wapatao 80,000 kati ya wakimbizi wapatao 250,000 wa Palestina wanaoishi nchini Lebanon. Israel inashambulia mara kwa mara maeneo ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa haichukui hatua yoyote ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni kwa jinai zake hizo. 

Siku ya Jumapili, Israel ilishambulia gari katika eneo la Ayn al-Mizrab, kaskazini mwa Bint Jbeil huko kusini mwa Lebanon na kuua watu wawili. Kama ambavyo pia, Hazem Qassem, msemaji wa Hamas amewalaani wanajeshi wa Israel kwa kuendelea kuwalenga na kuwaua shahidi raia katika maeneo kama ya Khan Yunis huko Ghaza; jambo linalowalazimisha Wapalestina kuhama makazi yao.