Maandamano ya kuunga mkono Iran yamefanyika nchini Afrika Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137230-maandamano_ya_kuunga_mkono_iran_yamefanyika_nchini_afrika_kusini
Wananchi wa Afrika Kusini walifanya maandamano na mikusanyiko mikubwa wakionyesha uungaji mkono wao kwa Iran kufuatia uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-03-08T10:34:19+00:00 )
Mar 08, 2026 10:18 UTC
  • Maandamano ya kuunga mkono Iran yamefanyika nchini Afrika Kusini

Wananchi wa Afrika Kusini walifanya maandamano na mikusanyiko mikubwa wakionyesha uungaji mkono wao kwa Iran kufuatia uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa televisheni ya China, wananchi wa Afrika Kusini walikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Johannesburg, wakilaani jina za Marekani na Israel dhidi ya watu wa Iran.

Waandamanaji walitaka maafisa wa Marekani na wa utawala wa Kizayuni wa Israel wafikishwe mahakamani kwa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Iran na Gaza.

Katika maandamano hayo, wananchi wa Afrika Kusini pia walitoa heshima kwa  Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu), muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na kiongozi shahidi wa Mapinduzi Imam Khamenei aliyeuawa Jumamosi iliyopita katika hujuma ya pamoja ya Marekani na Israel.

Aidha wamesisitiza ulazima wa kuwaondoa wavamizi katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Waandamanaji walitangaza kuwa kujilinda ni haki halali ya Iran, na wakataka waliotekeleza uhalifu huo wawajibishwe na kulipia damu ya mashahidi.