Watunisia waunga mkono Iran na kulaani vita vya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137232-watunisia_waunga_mkono_iran_na_kulaani_vita_vya_marekani
Watunisia wamefanya maandamano ya kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kukosoa kauli ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ambayo haikulaani mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa la Iran.
(last modified 2026-03-08T08:00:36+00:00 )
Mar 08, 2026 08:00 UTC
  • Maandamano ya Watunisia
    Maandamano ya Watunisia

Watunisia wamefanya maandamano ya kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kukosoa kauli ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ambayo haikulaani mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa la Iran.

Waandamanaji wa Tunisia walikuwa na picha za kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran na Ismail Haniyeh, kiongozi wa zamani harakati ya Hamas aliyeuawa shahidi na utawala haramu wa Israel.

Vilevile wamepeperusha bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Palestina na Lebanon katika maandamano hayo.

Washiriki katika maandamano hayo wametoa wito wa kufanyika maandamano ya umma nchini Tunisia na katika nchi zote za Kiarabu ili kuunga mkono taifa la Iran.

Watunisia pia wamekosoa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ambayo haikutangaza mshikamano wake na Iran na badala yake imetosheka kutangaza uungaji mkono wake kwa nchi za Kiarabu.

Wamesema wanataraji kwamba bunge la nchi hiyo litachukua msimamo tofauti na kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kambi ya Muqawama na mapambano dhidi ya Marekani na Israel.