Niger yaguswa na mauaji ya kigaidi ya Kiongozi Muadhamu wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137178-niger_yaguswa_na_mauaji_ya_kigaidi_ya_kiongozi_muadhamu_wa_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger amelinyooshea mkono wa pole taifa la Iran kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
(last modified 2026-03-05T10:12:36+00:00 )
Mar 05, 2026 10:12 UTC
  • Niger yaguswa na mauaji ya kigaidi ya Kiongozi Muadhamu wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger amelinyooshea mkono wa pole taifa la Iran kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger ameutembelea ubalozi wa Iran katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika, na kusaini kitabu cha kumbukizi na kumuomboleza Kiongozi Muadhamu.

Marekani na Israel zilianzisha hujuma za kigaidi dhidi ya Iran Jumamosi tarehe 28 Februari na kumuua shahidi  Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, wakuu wengi wa kijeshi, na mamia raia wakiwemo watoto wadogo.

Mataifa mengi duniani yakiwemo ya Afrika yameguswa na kusikitishwa na mauaji ya kidhulma ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Hivi karibuni, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria alituma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Kwenye ujumbe huo, Sheikh Zakzaky alielezea hasara kubwa na maumivu yake kufuatia tukio hilo chungu huku akitangaza kufungamana na  familia ya Shahidi Imam Khamenei, wannazioni wa Kiislamu  na wananchi wa Iran, Ummah wa Kiislamu, na wanaodhulumiwa duniani. Amesema: “Mauaji haya ni kinyume cha ubinadamu na ya kiwoga ni hujuma ya wazi dhidi ya binadamu wote.”